Lakini tena, wakati wa kutazamia ukapita, na Mwokozi wao hakutokea. Sasa wakaona kama Maria alivyofanya wakati alipokuja kwa kaburi la Mwokozi na kukuta linapokuwa wazi, akapaza sauti na kulia: “Wameondoa Bwana wangu, wala sijui pahali walipomuweka.” Yoane 20:13. TSHM 192.4
Hofu kwamba habari ingeweza kuwa kweli ikatumiwa kama kizuio juu ya ulimwengu usiosadiki. Lakini walipoona hakuna alama za hasira ya Mungu, wakafunika tena hofu yao na kuendelea na laumu lao na cheko. Kundi kubwa lililojidai kuamini wakaacha imani yao. Wenye kuzihaki wakavuta wazaifu na wenye kuogopea vyeo na hawa wote wakajiunga katika kutangaza kwamba ulimwengu unaweza kudumu kwa namna ileile kwa maelfu ya miaka. TSHM 192.5
Waaminifu waliojitoakwa kweli walikuwa wameacha vyote kwa ajili ya Kristo, na kama walivyoamini, wakatoa onyo lao la mwisho kwa ulimwengu. Kwa hamu kubwa sana walikuwa wameomba , “Kuja Bwana Yesu.” Lakini sasa kwa kuchukua tena mzigo wa matata ya maisha na kudumu kwa matusi ya ulimwengu wenye kuzihaki lilikuwa jaribu la kutisha sana. TSHM 193.1
Wakati Yesu alipopanda juu ya punda na kuingia Jerusalem kama mshindi wanafunzi wake waliamini kwamba alitaka kuketi juu ya kiti cha ufalme cha Dawidi na kukomboa Israeli kwa magandamizi. Kwa matumaini ya juu, wengi wakatandika mavazi yao ya inje kama zulia (tapis) katika njia yake wala kutapanya mbele yake matawi yenye majani mengi ya ngazi. Wanafunzi walikuwa wakitimiza kusudi la Mungu,lakini wakaangamizwa kwa uchungu mkali. Lakini siku chache zikapita kabla hawajashuhudia kifo cha maumivu makubwa cha Mwokozi na kumlaza ndani ya kaburi. Matumaini yao yakafa pamoja na Yesu. Hata wakati Bwana alipofufuka toka kaburini ndipo wakaweza kufahamu kwamba mambo yote yalitabiriwa kwa unabii. TSHM 193.2