Go to full page →

Jerome Anatii Baraza TSHM 46

Mvunjo wa hati ya Huss ukaamsha zoruba ya hasira. Baraza ikakusudia kwamba, badala ya kuchoma Jerome, yafaa kumshurutisha kukana. Akapewa kuchagua kati ya mambo mawili kukana mambo ya kwanza au kufa juu ya mti. Alipo zoofishwa na ugonjwa, kwa ajali ya mitetemo ya gereza na mateso ya mashaka na wasi wasi, kutengana na marafiki, na kuhofishwa kwa ajili ya kifo cha Huss, nguvu za Jerome zikafifia. Akakubali imani ya kikatolika na uamuzi wa baraza uliohukumu wycliffe na Huss, lakini akasimamia “kweli takatifu” walizofundisha. TSHM 46.1

Lakini katika upekee wa gereza lake aliona wazi jambo alilofanya. Aliwaza juu ya uhodari na uaminifu wa Huss na akafikiri kukana kwake mwenyewe kwa ukweli. Akafikiri habari ya Bwana Mungu ambaye kwa ajili yake mwenyewe alivumilia msalaba. Kabla ya kukana kwake alipata usaada ndani ya mateso katika hakikisho la wapenzi wa Mungu, lakini sasa majuto na mashaka yakatesa roho yake. Alijua kwamba mambo ya kujikana kwingine yalipaswa kufanywa kabla ya yeye kuweza kuwa na amani pamoja na Roma. Njia ambayo aliingia ilipaswa kuishia tu katika ukufuru kamili. TSHM 46.2