Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. Warumi 13:12 Mar 107.1
Wakati huu, tunapaswa kuwa na shabaha moja mbele yetu - kuwekeza kila alichokitoa Mungu kwa ajili ya kupandikiza kweli katika mioyo ya watu. . .Ni wajibu wa kila Mkristo kupambana kwa uwezo wote alio nao ili kusambaza ujuzi wa ukweli. Mar 107.2
Mungu amesubiri kwa muda mrefu, na bado anangoja, kuwa na wale ambao ni wake kwa njia ya uumbaji na pia ukombozi. Shauku yake ni kwamba waisikilize sauti yake, wamtii Yeye kama watoto wenye upendo na wanyenyekevu, ambao tamaa yao ni kuwa karibu naye, na kung’aa kutokana na mwonekano wake juu yao. Tunapaswa kupeleka ujumbe wa malaika yule wa tatu kwa ulimwengu na kuwaonya watu dhidi ya ibada ya mnyama na sanamu yake, na kuwaelekeza kuchukua nafasi zao katika safu ya wale “wazishikao amri za Mungu, na kuwa na imani ya Yesu.” Mungu hajafunua kwetu wakati ujumbe huu utakapofungwa, au wakati rehema itakapokwisha. . . Ni wajibu wetu kusubiri na kufanya kazi na kungoja, kutenda kazi kila wakati kwa ajili ya roho za watu walio katika uangamivu. . . Mar 107.3
Sasa, hivi sasa, ni wakati wa kukesha, kufanya kazi, na kungoja. . . .Mwisho wa mambo yote umekaribia. . . Roho wa Bwana anafanya kazi ya kuchukua ukweli wa Neno lilovuviwa na kulitia ndani ya kila roho ili wale wajiitao kuwa wafuasi wa Kristo wawe na furaha iliyo takatifu, ambayo itawawezesha kuambukiza wengine. . . Mar 107.4
Lipo hitaji la kuwa na ushuhuda, ulio wa kina zaidi, ulio na nguvu zaidi unaohusu ukweli kama unavyoonekana katika utauwa halisi wa wale wanaodai kuuamini. Mar 107.5
Tunapaswa kupandikiza kweli katika mioyo, na pia kufundisha wengine kama hiyo kweli ilivyo katika Yesu. Ulimwengu umo katika wakati mzito sana; roho zimo katika kuamua hatima yao ya milele. Shetani pamoja na malaika zake wanadumu katika kupanga namna ya kufanya sheria ya Mungu isiwe ya maana kwa watu, na kwa namna hiyo kuteka roho zao na kuwaingiza katika taabu ya dhambi. Kiza kinachoifunika dunia kinazidi kuongezeka, bali watembeao kwa unyenyekevu na Mungu hawana cha kuwatisha. Mar 107.6