Marabi walishikilia nafasi ya kumshitaki Yesu, lakini walitafuta kutimiza jambo hilo kupitia kwa wanafunzi wake. Kwa njia ya kuwachochoea wawe na chuki, walitumaini kuwafarakanisha na Bwana wao. Walisema: “Kwa nini Bwana wenu hula na watoza ushuru, na wenye dhambi?” TVV 148.1
Yesu hakungoja wanafunzi wake wawajibu, ila Yeye mwenyewe aliwajibu, akisema:.... Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.” Mafarisayo walijidai kuwa wenye haki, kwa hiyo hawakuhitaji tabibu, lakini waliwahesabu watoza ushuru na watu wa mataifa kuwa wapotevu. Basi haikuwa kazi yake kama tabibu kuwaendea watu wasiomhitaji, ila wanaomhitaji. TVV 148.2
Yesu akawaaambia Marabi: “Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya. Nataka rehema wala si sadaka.” walijidai kulielewa neno la Mungu, lakini kamwe hawakuifahamu tafsiri yake kiroho. TVV 148.3
Mafarisayo walinyamazishwa kwa muda, lakini walikusudia kamili kuendeleza uadui wao juu ya Yesu. Mara tena walijaribu kuwachochea wanafunzi wa Yohana Mbatizaji juu ya Yesu. Mafarisayo hao walikuwa wamemdharau Yohana mbatizaji kwa ajili ya maisha yake ya kutotaka makuu, na mavazi yake hafifu. Walimwita kuwa mtu aliyepungukiwa na akili. Walikuwa wamejaribu kuwachochoea watu wasimjali. Roho wa Mungu alikuwa amewaingia watu hawa wenye kudharau, wakatubu na kuungama dhambi zao, lakini walitangaza kwaamba Yohana ana roho wa mashetani. TVV 148.4
Sasa Yesu alipokuja akichanganyikana na watu, na kula pamoja nao, na kunywa nao, wakamshitaki kuwa mlafi na mlevi. Hawakudhani kuwa Yesu alikula na wenye dhambi ili awalete nuruni, awatoe gizani. Hawakudhani kuwa kila neno lililonenwa na Mwalimu wa mbinguni, ilikuwa mbegu iliyopandwa, ambayo itaota na kuzaa matunda kwa utukufu wa Mungu. Wao hawakukusudia kuipokea nuru hiyo, na ijapokuwa walimdhihaki Yohana Mbatizaji, sasa hawakutaka kufanya urafiki na wanafunzi wake ili kumpinga Yesu. Walisema kuwa Yesu alikuwa anadharau mapokeo yao ya kale, walitofautisha hali ya Yohana na kuona kuwa ilikuwa nafuu kuliko hii ya Yesu ya kula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi. TVV 148.5
Kwa wakati huu wanafunzi wa Yohana walikuwa na huzuni sana. Siku zao zilikuwa za maombolezo kwa vile Mwalimu wao mpendwa alikuwa gerezani. Na Yesu hakufanya chochote ili kumsaidia. Kama Yohana alitumwa na Mungu, kwa nini Yesu na wanafunzi wake wanatofautiana basi? TVV 148.6
Wanafunzi wa Yohana walidhani kuwa, huenda kuna haki katika maneno ya mafarisayo. Waliona kanuni nyingi zilizoshikwa na Marabi. Kufunga kulikuwa tendo linaloenea kwa Wayahudi, nalo lilionyesha wema, ambalo lilitendwa mara mbili kila juma. Mafarisayo na wanafunzi wa Yohana walikuwa wakifunga, wakati wanafunzi wa Yohana walipomjia Yesu na swali: “Kwa nini sisi na Mafarisayo hufunga kila mara, bali wanafunzi wako hawafungi?” TVV 149.1
Yesu alijibu kwa upole. Hakutaka kukanusha kawaida yao juu ya kufunga, ila kuwaelekeza vizuri, kuhusu kazi yake. Yohana mwenyewe alikuwa amesema: “Aliye na bibi arusi ndiye bwana arusi, asimamaye na kumsikia akifurahia sauti ya bwana arusi; kwa hiyo furaha yangu ni kubwa.” Yohana 3:29. Wanafunzi wa Yohana hawakusahau maneno ya Mwalimu wao. Kwa kutoa kielelezo Yesu alisema: “Mwaweza kuwafanya watoto wa bibi arusi wafunge wakati bwana arusi yuko pamoja nao?” TVV 149.2
Mkuu wa mbinguni alikuwa pamoja na watu. Zawadi kuu ya Mungu imetolewa kwa ulimwengu. Furaha kwa maskini kwa sababu amekuja kuwafanya warithi katika ufalme wake. Furaha kwa matajiri, kwa sababu atawafundisha kusalimisha mali yao; ya milele. Furaha kwa wajinga, kwa sababu ataelimisha hata wapate wokovu. Furaha kwa wenye elimu, kwa sababu atawafungulia kina kipana zaidi cha mambo ambayo hawajayaona. Huu sio wakati wa kulia kwa wanafunzi na kufunga. Lazima wafungue mioyo yao wapokee utukufu wake, ili nao wapitishe nuru hiyo kwa wale wanaoishi gizani na katika uvuli wa mauti. TVV 149.3