“Wa heri wenye upole”. Mambo magumu tunayopata yanaweza kupunguzwa kwa ajili ya upole uliofichika ndani ya Kristo. Tukiwa na unyenyekevu wa Bwana wetu, tutashinda, mapingamizi yote, na uchokozi wote. Mambo kama hayo hayataweza kuleta wasiwasi na giza katika moyo. Mtu anayeshindwa na mapingamizi ya kila namna hawezi kuwa na utulivu wa moyo, naye humwibia Mungu haki yake ya kudhihirisha tabia yake ndani ya mtu. Upole wa roho ni uwezo unaoleta ushindi kwa wafuasi wa Kristo. TVV 163.2
Wale wanaoonesha roho ya upole ya Kristo, wanaweza kuonekana kwa watu wa dunia kama watu duni, wanaodharauliwa lakini mbele za Mungu ni wenye thamani sana. Maskini wa roho, wanyenyekevu wa roho, ambao kusudi lao kubwa ni kufanya mapenzi ya Mungu, watahesabika katika kundi ambalo limefua mavazi yao na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana Kondoo. TVV 163.3
“Wa heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa” kule kujisikia kutofaa kwa mtu kutamfanya mtu awe na njaa kwa ajili ya haki. Wote wanaotamani kupata tabia sawa na ya Mungu watatosheka. Upendo utaufanya moyo wa mtu uchuchumilie mambo ya juu, na wala mtu hatakoma wala kuridhika na mambo hafifu yasiyotimilika. TVV 163.4
Wenye rehema watarehemiwa, na wenye moyo safi watamwona Mungu.. Kila mawazo machafu hutia hali ya tamaa mbaya na kumfukuza Roho Mtakatifu. Bwana anaweza kumsamehe mwenye kutubu, walakini ingawa amesamehewa, roho yake imeharibiwa. Usemi wote mchafu, na mawazo yote machafu, lazima viepukwe na mtu anayetamani kufahamu mambo ya mbinguni, ambayo ni ukweli kamili. TVV 163.5
Lakini maneno ya Kristo, yanaenda zaidi ya kuacha mawazo machafu tu, au kawaida nyingine zisizo safi, ambazo Wayahudu waliziepuka. Ubinafsi hutuzuia tusimwangalie Mungu. Tusipouacha ubinafsi na kutafuta mambo ya ubinafsi, hatuwezi kumwelewa Mungu ambaye ni Pendo. Moyo usiokuwa na ubinafsi peke yake, na moyo mnyenyekevu unaotegemea maongezi ya Mungu, na moyo wenye rehema, ndio utamwona Mungu. Kutoka 34:6. TVV 163.6
“Wa heri wasuluhishi” Ulimwengu ni adui wa sheria ya Mungu. Wenye dhambi ni maadui wa Mwumbaji wao. Kwa hiyo matokeo yake huwa adui wao kwa wao. Mipango ya wanadamu itashindwa kuleta amani, kwa sababu mipango hiyo haitoki mioyoni. Uwezo peke yake unaoweza kuleta amani ni neema ya Kristo tu. Neema hii inapokaa moyoni, itafukuza maovu yote ya tamaa ya mambo ya ulimwengu inayochipuza mashindano na vita. TVV 164.1