Yesu alikuwa amiri jeshi huko mbinguni, na malaika walikuwa wakifanya mapenzi yake; na sasa alikuwa mtumishi mtiifu kazini. Alifanya kazi kwa mikono yake pamoja na Yusufu. Hakutumia miujiza ya mbinguni kumsaidia kufanya kazi. Alitumia nguvu za mwili, ili awe na afya ya kumwezesha kutenda kazi barabara. TVV 35.1
Hakuwa mzembe katika shughuli, hata kushika vyombo vya kazi ya useremala. Alikuwa kamili katika kazi kama alivyokuwa kamili katika tabia. Aliweka kielelezo kwamba kazi yapaswa kutendwa kwa ukamilifu, maana kazi ni kitu cha heshima. Mungu aliiweka kazi kuwa kitu cha mbaraka. Na mfanya kazi hodari tu ndiye anayepata furaha maishani. Mungu huwakubali watoto na vijana wanaofanya kazi kamili nyumbani kwao, huku wakishiriki mizigo ya kazi pamoja na baba zao na mama zao. Yesu alikuwa mwaminifu na hodari katika kazi. Alitarajia mambo makuu, kwa hiyo alijaribu mambo makuu pia. Alisema, “Inanipasa kufanya kazi zake aliyenipeleka, wakati kungali mchana.” Yohana 9:4. Yesu hakuepa kazi yoyote, au wajibu kama watu wengine wafanyavyo leo, huku wakijiita kuwa wafuasi wake. Kwa kuwa huepuka wajibu huu, watu wengi ni dhaifu, wala hawafai kitu, nao huonekana kutofaa wakati wa shida. Uhodari na uwezo ulioonekana kwa Kristo unaweza kuwa wetu pia, kwa kufuata hali ile ile Kristo aliyofuata. Neema aliyopata ni kwa ajili yetu. TVV 35.2
Mwokozi wetu alishiriki mambo mengi ya kimaskini. Wale wanaoelewa hali kamili ya Kristo, hawataona kuwa utajiri unafaa kuliko umaskini. TVV 35.3