Wayahudi mwaka wa kumi na mbili ulikuwa ndio mgawanyiko kati ya utoto na ujana. Katika kawaida hii, Yesu alikuwa na haki ya kwenda kuhudhuria pasaka pamoja na Mariamu mamaye, na Yusufu, maana alikuwa amefikisha umri unaotakiwa. TVV 37.1
Safari ya kutoka Galilaya mpaka Yerusalemu ilichukua sku kadhaa. Wasafiri iliwapasa kujiunga katika kundi kubwa ili kujilinda. Wanawake na wazee walipanda punda, au gari la kukokotwa na ng’ombe. Njia ilikuwa ya mitelemko na miamba. Watu wengine walitembea kwa miguu. Njiani kulikuwa na maua na hali safi, na nyimbo za ndege. Wazazi waliwaeleza watoto wao maajabu ya Mungu, kadiri wahvyosafiri. Maadhimisho ya pasaka yalianza tangu taifa la Israeli lilipotoka Misri kwenda Kanaani. Siku ya mwisho ya utumwa wao huko Misri, Mungu aliwaagiza Waisraeli kujikusanya, kijamaa na kuchinja mwana kondoo. Baada ya kunyunyiza damu ya kondoo katika vizingiti na miimo ya milango, basi walikula nyama ya kondoo iliyookwa na mikate isiyochachwa, na mboga chungu. “Hii ndiyo pasaka ya Bwana.” Kutoka 12:11. Panapo usiku wa manane wazaliwa wa kwanza wote wa Misri waliuawa. Ndipo Waebrania walitoka katika nchi ya Misri wakiwa taifa linalojitegemea. TVV 37.2
Pasaka ilifuatiwa na siku kuu ya muda wa siku saba. Siku kuu hiyo ilikuwa ya mikate isiyochachwa. Maadhimisho hayo yote yalionyesha kuja kwa Mwokozi. Kondoo wa kuchinjwa, mkate usiochachwa, malimbuko, vilionyesha Mwokozi. Lakini wakati wa Kristo, sikukuu hizo zote hazikuwa na maana yoyote, ilikuwa kawaida au desturi tu, iliyokuwa ikifanywa na watu. Haikuonyesha lolote kuhusu Mwana wa Mungu! TVV 37.3
Mara ya kwanza mtoto Yesu alilitazama hekalu. Aliwaona makuhani wenye kanzu nyeupe wakifanya huduma zao, mwanakondoo akilazwa madhabahuni akiwa ametolewa kuwa kafara. Aliona huduma ya pasaka ikifanywa kwa uzuri na utaratibu hasa. Kila siku aliona maana ya yote hayo kwa uwazi zaidi. Kila tendo lilielekea hasa juu yake. Mwamko mpya ulionekana kwake. Alijifunza katika hali ya kimya juu ya matatizo. Siri ya kazi yake ilifunuliwa kwake kama Mwokozi. TVV 37.4
Mawazo yake yalichangamka kwa maajabu ya mambo aliyoona, hata akawa kama mtu aliyepigwa bumbuazi, ila wenye kuabudu walipotoka na kwenda, alibaki nyuma akitafakari. TVV 38.1
Katika mkutano huu wa pasaka, wazazi wake walitaka kumleta Yesu kwa walimu wakuu wa Israeli. Walitamani apate kuadibika kutokana na walimu hawa wakuu. Lakini Yesu alifundishwa na Mungu hekaluni kuwa yale aliyopokea, lazima ayapitishe kwa wengine. TVV 38.2
Chumba kilichoungwa katika hekalu, kiliwekwa ili kiwe shule. Hapo mtoto Yesu aliingia na kuketi katika miguu ya walimu wakuu waliojifunza sana. Alikuwa akiwahoji maswali mbalimbali, kama mtu atafutaye hekima. Alikuwa akiwauliza mambo ya unabii na mambo yaliyotokea, kuhusu Masihi. TVV 38.3
Maswali yake yalieleza ukweli wa ndani; ambayo yalikuwa hayaeleweki, lakini yanahusu wokovu. Maswali yake yalionyesha jinsi walimu hawa walivyokuwa gizani, kuhusu unabii wa kuhusu kuja kwa Masihi. Walionekana kuelewa vipya kuliko jinsi walivyoelewa hapo mwanzo. Walimu hao walizungumza juu ya hali mpya ambayo italetwa na kuja kwa Masihi. Lakini Yesu alielekeza unabii wa Isaya unaotaja juu ya mateso ya Mwana Kondoo wa Mungu. Isaya 53. TVV 38.4
Walimu wakuu hawa, walimwuliza maswali, nao walishangazwa na majibu yake. Kwa unyenyekevu alieleza maana yake, ambayo wao hawakuwa na habari. Kama wangalifuata mwongozo wa unabii wangalikuwa na matengenezo halisi katika mambo ya dini wakati huu, na Yesu alipoanza huduma yake, wengi wangalikuwa tayari kumwamini. TVV 38.5
Walimu hawa waliona nuru ya unabii ndani ya mtoto huyu wa Galilaya. Walitaka kukanusha elimu yake, maana wao ndio wangempatia maarifa hayo. TVV 38.6
Maneno ya Yesu yaliwakoroga sana, ambavyo hawajakorogwa na maneno ya mtu yeyote. Mungu alikuwa akitaka kuwapa nuru kwa njia hiyo, ingawa walikuwa waongozi. Kama Yesu angalijaribu kuwafundisha, wangalimkatalia mbali. Lakini wao walijisifu kuwa ndio wanamfundisha yeye, na kujaribu maarifa yake kuhusu maandiko. Upole wa Yesu na hali yake ya neema, vilipunguza chuki yao. Mawazo yao yalifunguliwa kuona neno la Mungu dhahiri, na Roho Mtakatifu alisema ndani yao na kuwaongoza. TVV 38.7
Waliona kuwa matazamio yao ya kuhusu Masihi hayakuwa ya kufuatana na unabii, lakini hawakukubali kuwa walitafsiri unabii vibaya. TVV 39.1