Go to full page →

Ufufuo wa wafu, fundisho lenye utata TVV 338

Baina ya Mafarisayo na Masadukayo, fundisho la ufufuo wa wafu lilikuwa jambo la utata mkubwa. Mafari-sayo waliamini kabisa fundisho la ufufuo wa wafu, lakini fikara zao kuhusu hali ya baadaye ya wafu zilikuwa na kasoro. Mauti ilikuwa siri isiyoelezeka. Mabishano baina ya makundi hayo mawili yalizusha ubishi wenye hasira. TVV 338.3

Watu wa kawaida hawakuvutiwa na Masadukayo. Lakini wengi wa Masadukayo walikuwa na mvuto uletwao na utajiri wa mali. Katika hao ndio alichaguliwa kuhani mkuu. Kule kustahili kushika wadhifa huo kulitoa mvuto kwa mafundisho yao yenye makosa. TVV 338.4

Masadukayo waliyakataa mafundisho ya Yesu; mafundisho yake kuhusu maisha ya baadaye yalikuwa kinyume na dhana zao. Waliamini kuwa baada ya kuumbwa na Mungu mwanadamu aliachwa tu ajitawale. Walichukulia kuwa mwanadamu alikuwa huru kumudu mambo yake duniani, na hali yake ya baadaye imo mikononi mwake. TVV 338.5