Go to full page →

Wanafunzi Wakata Tamaa TVV 438

Matumaini ya wanafunzi yalitoweka wakati Kristo alipokufa. Mpaka mwisho hawakuwa wameamini kuwa atakufa; sasa iliwawia vigumu kuamini amekufa. Wakiwa wamelemewa na huzuni hawakuweza kufarijika kwa neno lo lote Yesu alilolisema. Imani yao kwa Yesu ilikuwa imepotea kabisa, lakini walikuwa hawajapata kumpenda Bwana wao kama sasa au kujisikia hitaji la kuwako kwake. Wanafunzi wa Kristo walitamani sasa kumpatia mazishi ya heshimu, ila hawakufahamu jinsi ya kufanya hivyo. Watu waliouawa kwa sababu ya uhaini dhidi ya serikall ya Warumi walizikwa katika ardhi ya kuzikia waalifu. Yohana na wanawake kutoka Galilaya wasingeweza kuuacha mwili wa Bwana wao ushughulikiwe na askari wasiyo na huruma na kuzikwa katika kaburi lisilo na heshima. Walakini hawakuweza kupata upendeleo wo wote kutoka kwa viongozi wa Wayahudi na wala hawakuwa na ushawishi wo wote na Pilato. TVV 438.3

Katika hali isiyotazamiwa, Yusufu wa Arimathaya pamoja na Nikodemo walijitokeza kutoa msaada kwa wanafunzi. Wote walikuwa wajumbe wa Baraza kuu la Kiyahudi (Sanhedrini,) wote walikuwa matajiri na walioheshimiwa, na wote walifahamiana na Pilato. Waliazimia kwamba mwili wa Yesu upate mazishi ya heshima. TVV 438.4