Adamu na Hawa waliposikia ahadi ya Mwokozi atakayekuja, walimtazamia kwa upesi sana. Walimpata mtoto wao wa kwanza, wakitumaini kuwa huenda yeye ndiye Mkombozi. Lakini hao waliopata ahadi ya Mkombozi, walikufa bila kuona matimizo ya ahadi hiyo. Ahadi ilirudiwa kusemwa tena kwa wazee na manabii, ili kuifanya upya. Hata hivyo hakuja. Unabii wa Danieli ulitaja wakati wa kuja kwake, lakini ujumbe wake haukutafsiriwa wote vyema. Karne na karne zilipita. Na mkono wa mtesi ulizidi kuwa mzito kwa Waisraeli, na watu wengi walikuwa tayari kusema, “Siku zinakawia, na njozi haitimizwi.” Ezekieli 12:22. TVV 17.1
Lakini kama nyota katika mzunguko wake, kama ilivyoamuriwa, kusudi la Mungu halijui kuharakisha, wala kuchelewa. Katika baraza la mbinguni, kuja kwa Kristo kuliamuliwa na kupangwa hasa. Wakati saa kuwa ya mbinguni itakapotima, Yesu, ambaye ni Masihi atazaliwa katika Bethlehemu. TVV 17.2
“Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwana wake.” Wagalatia 4:4. Ulimwengu ulikuwa tayari kwa kuja kwa Mkombozi. Mataifa yalikuwa yameunganika chini ya serikali moja. Lugha moja ilijulikana kila mahali. Wayahudi wote toka kila mahali walikusanyika Yerusalemi kwa sikukuu yao ya kila mwaka. TVV 17.3
Watu hawa waliporudi mahali pa mtawanyiko wao walipeleka habari za kuzaliwa kwa Masihi ambaye amekuja. TVV 17.4
Desturi ya kikafiri ilikuwa ikitoweka katika watu. Watu walitamani dini itakayowaridhisha. Watu waliokuwa wakitaka kujua zaidi, walikuwa wakimtafuta Mungu, ili wapate kuelewa yatakayotokea, baada ya kufa. TVV 17.5