Go to full page →

Wakati Kazi za Mama Zipaswapo Kupunguzwa KN 159

Ni kosa lifanywalo kwa kawaida kutotofautisha katika maisha ya mwanamke wakati akaribiapo kuzaa watoto. Wakati huo kazi ngumu za mama yapasa zipunguzwe. Mabadiliko makubwa yanafanyika mwilini mwake. Inatakiwa damu nyingi, na kwa hiyo nyongeza ya chakula kifaacho mwilini ili kuongeza damu hutakikana, Kama hapati chakula kifaacho kuulisha mwili, hawezi kuwa na nguvu za mwilini na mtoto wake hunyang’anywa nguvu. KN 159.4

Mavazi yake pia huhitaji kuangaliwa. Uangalifu mwingi ungetumiwa kuutunza mwili wake usipatwe na baridi. Asiulazimishe mwili kujihifadhi wenyewe bila lazima, kwa kukosa mavazi. Kama mama akikosa kupata chakula kizuri cha kutosha chenye kuulisha mwili atapungukiwa na damu nzuri, mwendo wa damu yake utakuwa dhaifu, na mtoto wake atakosa kuwa na vitu hivyo pia. Mtoto atashindwa kujitwalia mwilini mwake sehemu ya chakula inayobadilika kuwa damu nzuri kuulisha mwili. Siha ya mama na mtoto hutegemea sana mavazi mazuri ya joto na chakula cha kufaa mwilini. KN 159.5