Go to full page →

Kutojali Vitu vya Lazima Si Uwekaji Akiba KN 176

Mungu hatukuzwi mwili unapoachwa kwa uzembe, au kutotunzwa, hata usifae kwa kazi ya Mungu. Kuutunza mwili kwa kuupatia chakula cha kuulisha na kuutia nguvu ni mojawapo ya kazi za kwanza za mwenye nyumba. Afadhali kuwa na nguo na vyombo visivyo vya bei kubwa kuliko kujinyima chakula. Watu wengine hupunguza vyakula vya watu wa nyumbani ili kuweza kuwakaribisha wageni kwa njia ya kitajiri. Hii si busara. Katika kuwakaribisha wageni pasiwepo anasa. Mahitaji ya watu wa nyumbani yaangaliwe kwanza. Uwekevu usio na maana na desturi za kubunibuni tu mara nyingi huzuia ukarimu unapotakiwa na ambapo ungekuwa mbaraka. Kiasi cha chakula mezani mwetu kingekuwa cha kutosha ili hata akifika mgeni asiyetazamiwa aweze kukaribishwa pasipo kumtwisha mama mwenye nyumba mzigo wa kupika kingine. 7MH 322; KN 176.5

Uwekaji akiba siyo uchoyo, bali kutumia mali kwa akili kwa sababu kuna kazi kubwa ya kufanywa. Mungu hataki watu wake wajinyime kile ambacho ni lazima kwa afya na raha yao, lakini hapendezwi na upotevu wa mali, gharama kubwa kupita kiasi, ama kufanya ufahari. 8378, 379; KN 177.1