Go to full page →

Hali za Nchini Zipasazo Kufikiriwa KN 269

Huku tukipingana na ulafi na ulevi, hatuna budi kutambua hali inayowatawala wanadamu. Mungu amewajalia riziki wale wanaoshi katika nchi mbalimbali ulimwenguni. Wale wanaotamani kuwa watenda kazi pamoja na Mungu hawana budi kufikiri kwa uangalifu kabla ya kuainisna vyakula ambavyo wamepaswa kula na vile wasivyopaswa kula. Yatupasa kuhusiana na jamii. Matengenezo ya afya katika hali yake izidiyo kiasi yangefundishwa kwa wale ambao hali zao huwazuia kuyaiga, badala ya faida yangeleta madhara makubwa zaidi. Nikihubiri Injili kwa maskini, nimeamriwa kuwaambia kula chakula chenye kutia afya. Siwezi kuwaambia: “Msile mayai, wala mziwa, wala mafuta ya maziwa. Msitumie siagi kwa kupikia chakula.” Injili haina budi kuhubiriwa kwa maskini, lakini wakati haujafika bado kuamuru chakula halisi kabisa. KN 269.1