Go to full page →

Sura Ya 16 - Kuondoa Vuzuizi Vya Umoja kati ya Mungu na Mwanadamu KN 117

MISHIPA ya fahamu ya ubongo ambayo hupelekea habari mwili mzima ndiyo njia tu ambayo kwayo Mungu aweza kupelekea habari kwa mwanadamu na kuyabadili maisha yake ya moyoni kwa undani. Lo lote linalozuia mwendo wa upesi mno katika mishipa ya fahamu hupunguza nguvu na uwezo wa maana, na matokeo yake ya baadaye ni kuzidhooiisha akili za moyoni. 12T 347; KN 117.1

Utovu wa kiasi wa namna iwayo yote hupoozesha viungo vya fahamu na kudhofisha uwezo wa ubongo hata mambo yadumuyo milele yakawa hayathaminiwi, bali hulinganishwa na mambo ya kawaida. Uwezo bora zaidi wa akili, uliokusudiwa kwa makusudi bora, hutekwa nyara kwa tamaa mbaya zaidi. Kama mazoea yetu ya mwili si mema, uwezo wa akili na tabia ya moyoni hauwezi kuwa wenye nguvu; maana kuna ushirika mkuu baina ya mwili na tabia ya moyoni. 23T 50,51: KN 117.2

Shetani hufurahi kuona wanadamu wakijitumbukiza ndani zaidi kwenye taabu na mashaka. Ajua kuwa watu wenye mazoea mabaya na miili dhaifu, hawawezi kumtumikia Mungu kwa bidii, kwa moyo wa kuendelea, na safi kama wenye nguvu. Mwili wenye ugonjwa huwa na matokeo yanayoonekana katika ubongo. Kwa akili twamtumikia Bwana. Kichwa ni boma la mwili. Shetani hushinda katika kazi ya uharibifu aifanyao kwa kuwaongoza wanadamu kujifurahisha kwa mazoea yanayowaangamiza, na kujiangamiza wao kwa wao; maana kwa njia hii humnyang’anya Mungu ibada inayomstahili. KN 117.3

Shetani daima yu macho kuwaweka kabisa wanadamu chini ya utawala wake. Uwezo wake mkubwa sana juu ya mwanadamu ni kwa njia ya tamaa ya chakula, na hii hujaribu kuitamanisha kwa kila njia iwezekanavyo. 3Te 13, 14; KN 117.4