Go to full page →

Sura Ya 20 - Ndoa KN 144

MUNGU alimfanya mke kutoka kwa mume, awe mwenziwe na msaidizi wake akae pamoja naye, kumfurahisha, kumtia, moyo, na kumpendeza, naye mume amepaswa kuwa mzaidizi wake imara. Wote wanaoingia katika umoja wa ndoa wakiwa na kusudi takatifumume kuyapata mapenzi safi ya moyo wa mke, na mke kulainisha na kuikuza vizuri tabia ya mumewe na kuikamilisha hulitimiza kusudi la Mungu kwao. KN 144.1

Kristo hakuja kutangua kawaida hii, bali kuirudishia hali ya utakatifu na ubora lliyokuwa nayo mwanzoni. Alikuja kumrudishia mwanadamu tabia ya uadilifu ya kufanana na ile ya Mungu, naye alianza kazi yake kwa kuihalalisha ndoa. KN 144.2

Yeye ambaye alimpa Adamu mke, yaani, Hawa awe msaidizi wake alifanya mwujiza wake wa kwanza katika karamu ya arusi. Katika jumba la karamu mahali ambapo jamaa walifurahi pamoja, hapo naipo Kristo alipoanza kazi yake kwa watu. Hivyo alitoa idhini yake kwa ndoa, akionyesha kuwa ni desturi ambayo yeye mwenyewe alianzisha. Aliamuru ili wanaume na wanawake waungane katika ndoa takatifu, na kuwalea watoto ambao, wakiheshimiwa, wangejulikana kama watu wa jamaa ya nyumba ya Mbinguni. KN 144.3