Go to full page →

Manufaa ya Ndoa KN 152

Wanaojidai kuwa Wakristo wangefikiri sawasawa matokeo ya kila jambo zuri la ndoa, na kanuni takatifu ingekuwa msingi wa kila iambo litendwalo nao. Wazazi wengi wametumia vibaya majaliwa yao mema ya ndoa, na kwa kuzoea kujifurahisha kwa anasa wametia nguvu tamaa zao za mwili. (Wakati mwingine Ellen White husema habari za “siri na manufaa ya ngono”) Kuzidi mno katika neno hili lililo halali ndiko kunakolifanya liwe dhambi kubwa. KN 152.5

Wazazi wengi hawana maarifa wapaswayo kuwa nayo katika maisha ya ngono. Hawakukingwa Shetani asije akawashinda na kuzitawala nia zao na maisha yao ya ngono na kujizuia ataka wayatawale maisha yao ya ngono na kujizuia wasiwe na hali iwayo ya kutokuwa na kiasi. Lakini wengi hawaoni kuwa ni wajibu wa dini kuzitawala tamaa zao mbaya. Wamejiunga katika ndoa kwa kusudi lao wenyewe na, kwa hiyo, huflkiri kuwa ndoa huhalalisha uzoefu wa kujifurahisha kwa tamaa mbaya zaidi. Hata wanaume na wanawake wanaojidai kuwa watauwa hushindwa kujizuia, nao hujitoa kwa tamaa zao mbaya wala hawafikiri kuwa Mungu huwahesabia hatia kwa kutumia vibaya nguvu za uhai, na kuudhoofisha ama kuuondolea mwili mzima nguvu, au kuyakatisha maisha yao. KN 153.1