Kule Scandinavia ujumbe wa kurudi kwa Kristo ulihubiriwa pia. Wengi walichochewa kuungama na kuziacha dhambi zao na kutafuta msamaha katika jina la Kristo. Lakini wachungaji wa kanisa la taifa walizipinga harakati hizo, na baadhi ya watu waliokuwa wanahubiri ujumbe huo walitupwa gerezani. Katika sehemu nyingi ambapo wahubiri wa ujio wa Bwana ulioukuwa umekaribia walinyamazishwa, Mungu alipendezwa kupeleka ujumbe huo kwa kutumia watoto. Kwa kuwa walikuwa chini ya umri wa kushtakiwa, serikali haikuweza kuwazuia na waliruhusiwa kunena bila kusumbuliwa. TK 232.3
Katika makazi duni ya wafanyakazi, watu walikusanyika kusikiliza maonyo. Baadhi ya hao watoto waliohubiri walikuwa si zaidi ya miaka sita au minane; na wakati maisha yao yalishuhudia kuwa walikuwa wanampenda Mwokozi wao, na kwa kawaida walionesha akili nauwezo usio wa kawaida kwa watoto wa umri huo. Hata hivyo, walipokuwa wamesimama mbele ya watu, waliwezeshwa na uwezo uliokuwa zaidi ya vipaji vyao vya asili. Sauti zao na jinsi ya uzungumzaji vilibadilika, na walitoa onyo juu ya hukumu kwa uwezo mkubwa, “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja.” TK 232.4
Watu walipokea ujumbe huo kwa kutetemeka. Roho wa Mungu aliongea na mioyo ya watu. Wengi waliongozwa kuyatafuta Maandiko, wapenda anasa na waasheratiwalibadili mienendo yao, na kazi kubwa ya matengenezo ilifanyika kiasi kwamba hatamakasisi wa kanisa la nchi hiyo walilazimika kukiri kwamba mkono wa Mungu ulikuwa unaongoza harakati hizo. TK 233.1
Ulikuwa ni mpango wa Mungu kwamba habari njema za kurudi kwa Kristo zihubiriwe kule Scandinavia, hivyo akaweka Roho wake ndani ya watoto ili kazi hiyo ipate kutimizwa. Wakati Yesu alipokuwa anaingia Yerusalemu, watu waliokuwa wakimshangilia, walilazimika kutulia walipolikaribia lango la mji, kwa sababu waliwaogopa makuhani na wakuu. Lakini watoto waliokuwa kwenye nyua za hekalu waliendeleza nyimbo hizo wakisema, “Hosana, Mwana wa Daudi!” Mathayo 21:8-16. Kama Mungu alivyofanya makuu kwa kutumia watoto wakati wa ujio wa kwanza Wakristo, vivyo hivyo alifanya makuu kwa kutumia watoto kwa kuwakabidhi ujumbe wa ujio Wakristo. TK 233.2