Kadiri upinzani unavyoinuka katika viwango vya juu vya ukali, watumishi wa Bwana watafathaishwa tena, kwa sababu itaonekana kwao kuwa wameleta zahama. Lakini dhamiri zao na Neno la Mungu vitawathibitishia kwamba msimamo wao ni sahihi. Imani na ujasiri wao vitainuka tayari kwa ajili ya wakati wa hatari, ushuhuda wao ni “Kristo amezishinda nguvu za dunia, na je, tutaiogopaje dunia ambayo tayari imeshindwa?” TK 367.4
Hakuna mtu awezaye kumtumikia Mungu pasipo kusimama kinyume na upinzani wa majeshi ya giza. Malaika waovu watamshambulia, wakitambua kwamba mvuto wake unachukua mawindo kutoka mikononi mwao. Watu waovu watajitahidi kumtenganisha na Mungu kwa kumshawishi kwa majaribu makali. Ikiwa hawatafanikiwa kwa njia hizi nguvu itatumika kuilazimisha dhamiri. TK 368.1
Lakini kadiri Yesu anavyoendelea kuwa mpatanishi wa mwanadamu katika patakatifu pa mbinguni, nguvu ya ushawishi ya Roho Mtakatifu inatenda kazi kwa watawala na watu. Wakati wengi wa watawala wetu ni mawakala hai wa Shetani, Mungu pia anao mawakala wake miongoni mwa watu wanaoongoza mataifa. Watu wachache watasimama kupinga wimbi lenye nguvu la uovu. Upinzani wa maadui wa kweli utadhibitiwa ili ujumbe wa malaika wa tatu ufanye kazi yake. Onyo la mwisho litavuta usikivu wa viongozi hawa, na baadhi wataupokea na kusimama na watu wa Mungu katika wakati wa taabu. TK 368.2
Mvua ya Masika na Kilio Kikuu TK 368.3
Malaika anayeungana na malaika wa tatu ataiangazia dunia yote kwa utukufu wake. Ujumbe wa malaika wa kwanza ulipelekwa katika kila kituo cha utume duniani, na katika baadhi ya nchi kulikuwa na mwitikio mkubwa wa kidini ulioshuhudiwa tangu wakati wa Matengenezo. Lakini matokeo haya yatapitwa na onyo la mwisho la malaika wa tatu. TK 368.4
Kazi itakuwa kama ile ya kipindi cha Pentekoste. “Mvua ya vuli” ilimwagwa katika kipindi cha ufunguzi wa Injili ili kuotesha mbegu ya thamani; kwa hiyo “mvua ya masika” itamwagwa wakati wa kufungwa kwa Injili ili kuivisha mavuno.. Hosea 6:3, Yoeli 2:23. Kazi kubwa ya Injili haitafungwa kukiwa na udhihirisho mdogo wa nguvu ya Mungu kuliko ilivyoshuhudiwa katika ufunguzi wake. Unabii uliotimia wakati wa mvua ya awaliwakati wa ufunguzi wa Injili utatimizwa tena katika mvua ya masika wakati wa kufungwa kwa Injili. hizi ndizo “nyakati za kuburudishwa” ambazo mtume Petro alizitazamia wakati aliposema “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifiitwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani.” Matendo 3:19,20. TK 368.5
Watumishi wa Mungu, nyuso zao ziking’aa kwa kujitoa wakfu, wataharakisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine kuutangaza ujumbe wa mbinguni. Miujiza itatendeka,wagonjwa wataponywa. Shetani pia atatenda kazi kwa miujiza ya uongo hata kushusha moto kutoka mbinguni.-Ufunuo 13:13 kwa hiyo watu wa dunia watapaswa wawe na msimamo. TK 369.1
Ujumbe hautahubiriwa kwa msingi wa hoja ila kwa ushawishi wa kina wa Roho wa Mungu. Hoja zilikuwa zimetolewa, machapisho yaliwapa mvuto, lakini wengi hawakuuelewa ukweli. Sasa ukweli utaonekana jinsi ulivyo.. Mwunganiko wa familia, mahusiano ya kanisa hayana nguvu sasa kuwazuia watoto waaminifu wa Mungu. Pamoja na kwamba mawakala wameungana dhidi ya ukweli, idadi kubwa watafanya uamuzi wao kuwa upande wa Bwana.(Tense) TK 369.2