Hatimaye viongozi katika mamlaka ya Papa walibadilisha mbinu na kutumia njia za kidiplomasia. Mwafaka ukafikiwa ambao uliwasaliti watu wa Bohemia wakaingia katika mamlaka ya Kanisa la Roma. Watu wa Bohemia waliweka mambo manne bayana kama masharti ya kupatana na Kanisa la Roma: TK 76.4
(1) Uhuru katika kuhubiri Biblia TK 76.5
(2) Haki kwa ajili ya kanisa zima kushiriki mkate na divai kwenye meza ya Bwana na matumizi ya lugha ya asili katika ibada kuu; TK 76.6
(3) Kuondolewa kwa viongozi wa kanisa kutoka katika ofisi zote na mamlaka za kiulimwengu; na TK 76.7
(4) Katika mazingira ya uhalifu, mamlaka ya kisheria ya mahakama za jamii yawe juu ya wachungaji na walei pia. Mamlaka ya pPapa ilikubali kuwa mambo hayo manne yakubaliwe, “lakini haki ya kuyaeleza iwe kwenye baraza-kwa maneno mengine, kwa Papa na kwa mfalme.” 33Ibid.y ch. 18. TK 76.8
Kanisa la Roma lilifanikiwa kwa njia ya unafiki na udanganyifu katika kile lilichoshindwa kukipata kwa njia ya vita. Kwa kuweka tafsiri zake yenyewe kwenye maandishi ya wafuasi wa Huss, kama ilivyofanya kwenye Biblia, ingefanikiwa kupotosha maana ili kupelekana na makusudi yake. TK 77.1
Kundi kubwa Bohemia, lilipoona kuwa uhuru wao umesalitiwa, halikukubaliana na mkataba. Mafarakano yakaanza, yaliyosababisha ugomvi kati yao wenyewe. Muungwana Procopius alishindwa, na uhuru wa Bohemia ukaisha. TK 77.2
Kwa mara nyingine, majeshi ya kigeni yalivamia Bohemia, na wale waliobaki wakiwa waaminifu kwa Injili walitoswa kwenye mateso ya umwagaji damu. Pamoja na hayo, uthabiti wao haukutingishika. Huku wakiwa wamelazimika kukimbilia mapangoni, waliendelea kukusanyika kwa ajili ya kusoma Neno la Mungu na kuungana katika kumw abudu yeye. Kwa njia ya wajumbe waliotumwa kwa siri kwenda nchi mbalimbali walifahamu kuwa “kati ya milima ya Alps kulikuwa na kanisa la kale, ambalo limejengwa katika misingi ya Maandiko, na kupinga upotovu wa Roma wa kuabudu miungu.” 34Ibid., ch. 19 Kwa furaha kuu, mawasiliano na Wakristo Wawaldensia yalianzishwa. TK 77.3
Wakiwa thabiti katika Injili, watu wa Bohemia walisubiri katika usiku wa mateso yao, katika wakati wa giza nene wakiendelea kukaza macho yao yaone upeo wake kama watu wanaoingoja asubuhi. TK 77.4