Kwenye moja ya shule za mji wa Paris, kulikuwa na kijana mmoja mwangalifu, mkimya na mwadilifu katika maisha yake, aliyekuwa na juhudi kwenye mambo ya kiakili na moyo wa kujitoa katika mambo ya dini. Kipaji alichokuwa nacho na jinsi alivyokuwa anakitumia vilimfanya awe fahari ya chuo chake, na John Calvin alikuwa anatazamiwa kwa matumaini kuwa mmoja wa watetezi wenye nguvu kabisa wa kanisa. TK 141.3
Lakini nuru ya Mungu ilipenya kuta za usomi na mapokeo potuvu ambazo zilikuwa zimemfunga. Binamu yake na Calvin aliyekuwa anaitwa Olivetan alikuwa amejiunga na Wanamatengenezo. Ndugu hawa walikuwa wanazungumzia mambo yaliyokuwa yanauvuruga Ukristo. “Kuna dini mbili tu duniani,” alisema Olivetan Mprotestanti. “Ile iliyoanzishwa na watu...ambamo watu wanajitumikia wenyewe kwa sherehe na matendo mema; nyingine ni dini iliyofunuliwa katika Biblia, inayomfundisha mwanadamu kutafuta wokovu bure kutoka kwenye neema ya Mungu peke yake.” TK 141.4
“Sitapokea lolote kati ya mafundisho yako mapya, unafikiri kuwa mimi nimeishi kwenye makosa siku zangu zote?” 137Ibid. bk. 13, ch. 7. Akiwa peke yake chumbani Calvin alikuwa anayafikiria maneno ya binamu yake. Aliona kwamba hakuwa na mtetezi mbele za Mungu mtakatifu na mwenye haki. Matendo mema, kawaida na desturi za kanisa vyote havikuwa na uwezo wa kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi. Kukiri imani ya kanisa, kitubio havikuwa na uwezo wa kumpatanisha mtu na Mungu. TK 141.5