Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura ya Saba—DALILI YA KUWA WANAFUNZI WAKE KRISTO

    “Mtu akiwa ndani ya Kristo, ni kiumbe kipya; vya kale vimepita; kumbe; vyote vimekuwa vipya.” 2 Wakor.5:17.HUK 25.1

    Pengine mtu hawezi kutaja siku wala mahali hasa alipoongoka kuwa mfuasi wa Kristo; lakini kukosa kufanya hivyo si kama kusema kwamba yule hakuongoka kweli. Kristo alimwambia Nikodemo, “Upepo huenda utakako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.” Yoh.3:8. Upepo hauwezi kuonekana, lakini twasikia na kuona matendo yake; na vilevile Roho ya Mungu ina julikana kwa namna ya matendo yake mioyoni mwa wanadamu. Uwezo wake, usioonekane na macho ya kibinadamu, huanzisha maisha mapya moyoni; humwumba mtu kuwa mpya kwa mfano wa Mungu. Ijapokuwa kazi ya Roho inatendeka kwa kimya, tena haionekani, matokeo yake yamekuwa waziwazi. Kama Roho Mtakatifu ametengeneza moyo kuwa mpya, jambo hilo litaonekana katika maisha yake aliyeongoka moyo. Ingawa sisi wenyewe hatuwezi kugeuza mioyo yetu, ama kujifanyiza nia zetu kupatana na Mungu; tena haifai kabisa kujitegemea wenyewe kwa matendo yetu yaliyo mema; walakini, kwa namna ya maisha yetu, itajulikana kama tunayo neema ya Mungu mioyoni mwetu. Itaonekana kwamba tabia zetu, desturi zetu, mazoezo yetu, na mambo yetu yote yamegeuka kuwa mbalimbali na yale ya zamani. Tabia na desturi za mtu fulani zinajulikana si kwa matendo mema au mabaya ya siku moja moja tu, ila kwa maelekezo ya matendo yake na maneno yake, na mazoezo yake ya sikuzote.HUK 25.2

    Ni kweli ya kuwa kuna watu ambao mienendo yao ni mema machoni pa wenzao, bila kuongoka moyo kwa ajili ya Kristo. Kwa sababu ya kupenda kusifiwa na kuwa kama waongozi kati ya wengine, hivyo hujilinda ili waonekane kuwa ni wenye adabu. Kwa ajili ya kujistahi nafsi yao, huyaepuka matendo mabaya ya nje. Hata mwenye kuzoea kujifikiria nafsi yake mwenyewe na kujipendeza, pengine anafanya mema. Ikiwa ni hivyo, twawezaje kuyakinisha kama tumekuwa upande wa Kristo, au sivyo ?HUK 25.3

    Ni nani anayeutawala moyo ? Fikara zetu juu ni ya nani ? Tunazoea kuzungumza juu ya nani ? Ni nani ambaye tunampenda zaidi na kumtumikia ? Ikiwa tu watu wa Kristo, fikara zetu ni juu yake. Tunajitoa kwake pamoja na vile tunavyo vyote. Twatake kufanana naye, kuwa na Roho yake mioyoni, kufanya mapenzi yake na kumpendeza kwa mambo yote.HUK 25.4

    Wale wanaokuwa wapya katika Kristo Yesu, hao nao watazaa matunda yo Roho, yaani, “upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi.” Wagal.5:22,23. Hawatafuata tamaa zao za zaraani, bali watamwamini Mwana wa Mungu na kufuata nyayo zake; tabia zake zitaonekana katika maisha yao, watatakaswa kuwa safi kama yeye alivyo mtakatifu. Mambo waliyochukizwa nayo zamani, sasa wanayapenda; na vile walivyopenda zamani, sasa huchukizwa navyo. Yule aliye fanya kiburi, sasa huwa mpole na mnyenyekevu. Mlevi huacha malevi yake, mwasherati na mzinzi huachana na matendo yao ya zamani, na kuwa watu safi. Mkristo hafuati anasa na mvao na mambo ya kidunia. Hataki kufanana na watu wa dunia kwa “kujipamba kwa nje,” “ila mtu wa moyoni asiyecnekana, katika jambo lisiloharibika; ni roho ya upole na utilivu iliyo ya thamani kuu mbele ya Mungu.” 1 Petro 3:3,4.HUK 25.5

    Kutubu si ya kweli isipokuwa imeonekana dhahiri kwamba mtu buongoka moyo na kufanya yaliyo mema. Kwama mtu anarudisha amana yake, na kutoa tena aliyoitwaa kwa unyang anyi, kuziungama dhambi zake, kumpenda Mungu na wenziwe, yule aliye mwenye dhambi anaweza kutumaini kwamba “amepita toka mauti hata uzima.” Yoh, 5:24,HUK 26.1

    Sisi wanadamu ambao tungali wabaya, tukimfikilia Kristo na kupata kusamehewa dhambi zetu, hali yetu inageuka kabisa. Upendo Auonekana moyoni. Twapata furaha katika kufanya yaliyo wajibu wetu sisi Wakristo; twapenda kujinyima kwa ajili yake Kristo. Zamani tulikuwa gizani, na sasa tuko katika nuru yake aliye “Jua ya haki,”HUK 26.2

    Tabia za Kristo zitaonekana katika wafuasi wake. Yeye alijitoa kufanya mapenzi ya Mungu kwa kuwa alimpenda Mungu.Mungu ni upendo. Upendo wa kweli hutoka kwa Mungu; pia unapatikana katika moyo ule tu ambao Yesu huutawala. Haupatikani kamwe katika moyo usioongoka na kujitoa kuwa wa Mungu. “Sisi twapenda kwa maana yeye kwanza alitupenda sisi.” 1 Yoh.4:19. Upendo wa Mungu ukiwa humo mioyoni mwetu, maisha yetu yatakuwa safi, hata wengine katika jirani zetu watavutwa moyo na kutaka kutongeneza maisha yao kuwa safi, hasa kwa ajili ya mfano mwema wao walio Wakristo wema.HUK 26.3

    Kuna makosa mawili ambayo watu wa Mungu hawana budi kuwa na kujihadhari nayo. Ya kwanza, kujitumainia matendo mema yao wenyewe ili wapatane na Mungu. Hakuna awezaye kujitakasa mwenyewo ila kwa njia ya kuamini neema na msaada wa Kristo.HUK 26.4

    Kosa la pili lipasalo sisi kuwa na hadhari nalo ni kinyumo cha lile la kwanza, ndilo kufikiri kwamba hatuna haja kuzishika sheria za Mungu; wengine hufikiri ya kuwa kama tumewekwa haki kwa neema ya Kristo tu, basi hakuna inayotakiwa juu yetu ili tupate wokovu katika Kristo. Lakini sivyo kabisa.HUK 26.5

    Angalia kwamba kumtii Mungu siyo kwa matendo ya nje yanayoonekana tu, bali kwa mambo ya moyo na upendo. Kumpenda Mungu ni asili ya kumtii. Iwapo upendo moyoni, tena mwanadamu ame- kuwa mpya katika mfano wa Yule aliyemwumba, ndipo inatimizwa ahadi ya agano jipya ya Mungu jinsi inavyoandikwa, “Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, na katika akili zao nitaziandika.” Waeb.10:16, Na sheria ikiwamo moyoni, itakuwa inaongoza katika mambo yote ya maisha ya mwanadamu. Kumtii Mungu kwa sababu ya kumpenda, hiyo ndiyo dalili ya kweli kama mtu fulani ni mfuasi wake. Imeandikwa hivi katika Biblia, “Huku ndiko kumpenda Mungu kuzishika amri zake.” “Yeye asemaye, Nimemjua, naye hazishiki amri zake, ni mwongo, na kweli haimo ndani yake.” 1 Yoh.5:3; 2:4. Hivyo twaona kwamba imetakiwa ili tumtii Mungu na kuzishika amri zake; lakini kwa kumwamini Kristo tu tutakavyoweza kumtii kwa njia ya kweli.HUK 26.6

    Hatuwezi kustahili wokovu kwa ajili ya utii wetu; wokovu ni thawabu ya Mungu iliyopewa bure, nasi tunaipokea kwa kumwamini Mungu. Na kumtii Mungu hufuatana na kumwanini. “Mhajua ya kuwa yeye alidhihiri ili aziondoe dhambi zetu; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yako hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona, wala hakumtambua.” 1 Yoh.3:5,6. Hiyo ndiyo dalili ya kweli inayodhihirisha kama mwanadamu ni mfuasi wa Kristo. Kama tunakaa ndani ya Kristo, na upendo wa Mungu hukaa mioyoni nwetu, ndipo mawazo na matendo yetu yatapatana na mapenzi yake Mungu jinsi yanavyonenwa katika amri zake takatifu. “Wanangu, mtu asikudanganyeni; afanyaye haki yuna haki; kama yeye alivyo na haki.” 1 Yoh.3:7. Namna ya haki inayotakiwa na Mungu imeelezwa kwa kipimo cha sheria yake, jinsi inavyonenwa katika zile amri kumi zilizotolewa na Mungu katika mlima wa Sinai.HUK 27.1

    Kusema ya kuwa tunamwamini Kristo, na huku kusema kwamba hatuna haja kumtii Mungu kwa mambo ya amri zake, hiyo si kuamini kwa kweli, bali ni kama kufanya kiburi tu, maana “mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani.” Waef.2:8. Lakini “imani isipokuwa na matendo, imekufa nafsini mwake. Yak.2:17. Na Yesu, kabla ya kuja kwake duniani, alisema, “Kufanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndio furaha yangu; na sheria yako imo ndani ya moyo wangu.” Zab.40:8. Tena kabla ya kurudi kwake mbinguni alisema, “Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu, na kukaa katika pendo lake.” Yoh.l5:10. Tena katika Maandiko imeandikwa hivi: “Na hivi twajua ya kuwa tumemjua, ikiwa tunashika amri zake.... Hivi twajua ya kuwa tumo ndani yake. Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vilevile kama yeye alivyoenenda.” “Maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akiwaacheni mfano,mfuate nyayo zake.” 1 Yoh.2:3-6; 1 Petro 2:21.HUK 27.2

    Sharti ya kupata uzima wa milele limekuwa moja tangu zamani,jinsi lilivyokuwa katika bustani ya Aden kabla Adamu na Hawa hawakuanguka na kufanya dhambi,ndilo hili, kumtii Mungu kwa ukamilifu katika mambo yote ya amri zake, kuwa na haki mkamilifu katika Kristo. Sisi peke yetu hatuna haki kabisa, ila kwa Kristo tu. Yesu alikaa hapa duniani, akajaribiwa kama sisi. Akaishi maisha yaliyo mkamilifu pasipo dhambi. Akafa kwa ajili yetu; akajitoa badala yetu; alikubali kuzichukua dhambi zetu ili sisi tupate kuwekwa haki kwake. Kama unajitoa kwake, na kumkubali kuwa ni Mwokozi wako, ijapokuwa umekuwa mwenye dhambi kabisa, utahesabiwa kuwa ni haki katika Kristo. Sifa njema ya Kristo itahesabiwa kuwa ni yako, nawe utakuwa katika hali ya kukubaliwa na Mungu kana kwamba hukufanya dhambi hasa.HUK 27.3

    Zaidi ya hayo, Kristo huigeuza hali ya moyo jinsi ulivyo. Hukaa ndani ya moyo wako kwa njia ya kuamini, Nawe umepaswa kuendelea kumwamini Kristo na kumtolea nia yako sikuzote ili upate kumshiriki Kristo daima; na kwa kadiri unavyoendelea kufanya hivyo, ndivyo atakavyotenda kazi ndani yako, ili kutaka kwako na kutenda kwako vipatane na kusudi lake jema. Ndipo utaweza kusema, “Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.” Wagal.2:20 Ndivyo Kristo alivyowaambia wanafunzi wake, “Kwa kuwa si ninyi msemao, bali Roho ya Baba yenu asemaye ndani yenu.” Mattayo 10:20. Na kama Kristo atenda ndani yako, utakuwa na nia sawa na nia iliyokuwamo ndani ya Kristo, na kutenda matendo kama vile alivyotenda yeye - matendo yaliyo ya haki, na kumtii Mungu.HUK 28.1

    Tukisema juu ya imani, lazima tufahamu ya kwamba kuna tofauti kati ya kusadiki tu ya kuwa Mungu yu hai, na kumwamini kabisa katika moyo. Hata Shetani na malaika wabaya kuamini kama Mungu yuko; huamini uwezo wake, na meneno yake jinsi yalivyo ya kweli: ni mambo wasiyoweza kukana. Biblia inasema, “Mashetani nao waamini na kutetemeka.” Yak.2:19; lakini hiyo siyo imani ya kweli. Mwaminifu wa kweli hujitoa kabisa kuwa wa Mungu na kufanya mapenzi yake. Kwa imani ya kweli moyo unatengenezwa kuwa upya kwa mfano wa Mungu. Moyo na nia ya mwili, iliyo katika hali ya zamani, haitli sheria ya Mungu wala haiwezi; bali yule aliyeongoka moyo, sasa hupata furaha katika amri zake, na kusema, “Nimeipendaje sheria yako! Ndio fikara yangu mchana kuchwa.” Zab.1l9:97. Na hivyo wema uagizwao na torati unatimizwa ndani yetu, tusioenenda“kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.” Warumi 8:4,1.HUK 28.2

    Kuna wengine ambao wamejua upendo wa Kristo na jinsi anavyowasamehe dhambi zao, nao wataka sana kuwa watoto wa Mungu; walakini waona ya kwamba sifa yao si kamili, na maisha yao si sawa. Hawo wamekaribia kuona shaka kama kweli mioyo yao imefanywa ipya na Roho Mtakatifu. Na wote wa kama hao nawaambia hivi, Msife moyo ninyi, wala kurudi nyume. Mara kwa mara tutalazimishwa kumwendea Yesu tukihuzunika kwa ajili ya makosa yetu; lakini haifai kushushwa moyo. Ingawa tumesliindwa na adui, Mungu hatatuacha na kututupia mbali. Sivyo; mtume Yohana aliandika, “Na ijapo mtu akatenda dhambi, tuna Mwombezi kwa Baba Yesu Kristo mwenye haki.” 1 Yoh.2:l. Tena tusisahau maneno yake Kristo,“Baba mwenyewe awapenda ninyi.” Yoh.16:37. Mungu anataka kukurudisha kwake mwenyewe, na kuona mfano wake ndani yako jinsi Yeye alivyo safi na takatifu. Endelea kuomba kwa moyo wa bidii zaidi; na kumwamini Mungu kabisa. Na kwa jinsi tunavyopungua kujitogemea uwezo wotu wenyewe, tuzidi kutegemea na kutumainia uwezo wa Mwokozi wetu na kumsifu.HUK 28.3

    Na kwa vile unavyozidi kumkaribia Yesu, hivyo utazidi kujion mwenyewe kuwa ni mwenye makosa zaidi; kwa kuwa macho ya kiroho yatazidi kuwa safi ya kufahamu namna ya ukosefu na upungufu wako, kwa vile unavyomtazama YESU na kujilinganisha naye jinsi alivyo mkamilifu.HUK 29.1

    Mtu asiyefahamu hali yake jinsi alivyo mbaya na mwenye dhambi, yule hawezi kumponda Yesu sana moyoni mwake; bali yule ambaye amaongoka moyo lava neoma ya Kristo, yeye atamheshimu Kristo kwa ajili ya sifa yake njema. Lakini isipokuwa tumefahamu hali yotu katika dhambi, tunabainisha ya kwamba hatujaona bado uzuri na ubora wake Kristo.HUK 29.2

    Kwa jinsi tunavyopungua kujiona bora wenyewe, hivyo tutakavyozidi kumheshimu Mwokozi wotu kwa wema na utakatifu wake. Mtu anapofahamu udhaifu wake na kumtaka Kristo, Kristo naye atamsaidia na kumjulisha uwezo wake. Na kwa vilo tunavyozidi kuona ubora na sifa yako Kristo, ndivyo tutazidi kuwa katika mfano wake.HUK 29.3

    Yosu kwetu ni Rafiki, hwambiwa haja pia;
    Tukiomba kwa Babaye, maombi asikia;
    Lakini twajikosesha, twajitweka vibaya;
    Kwamba tulimwomba Mungu, dua angesikia.

    Una dhiki na maonjo ? Una mashaka pia ?
    Haifai kufa moyo, dua atasikia.
    Hakuna mwingine Mwema, wa kutuhurmia;
    Atujua tu dhaifu; maombi asikia.

    Je, hunayo hata nguvu, huwezi kwendelea,
    Ujapodharauliwa, ujaporushwa pia.
    Watu wagekudharau, wapendao dunia,
    Hukwambata mikononi, dua atasikia.

    Bwana Yesu unitazame sasa,
    Unifanye niwe dhabihu hayi;
    Na jitoa kwako, na moyo, vyote;
    Unioshe sasa niwe mweupe.
    HUK 29.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents