Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uwezo katika Kitabu

    Dr. Wolff alisafiri katika inchi zilizokuwa za kishenzi kabisa bila ulinzi, kwa kuvumilia taabu na kuzunguukwa na hatari nyingi. Akateswa bila chakula, na baridi, kuuzwa kama mtumwa, mara tatu akakatiwa hukumu ya kifo, akaviziwa na wezi, na mara zingine karibu kufa kwa kiu cha maji. Mara moja akanyanganywa vyote na akaachwa na kusafiri mwendo wa mamia yakilometres kwa miguu katika milima, teluji zikipiga katika uso wake na nyanyo zisizo naviatu zikagandamizwa na udongo wa baridi sana.TSHM 172.5

    Walipomshauria kwamba si vema kusafiri bila silaha katika makabila yenye ukaidi na uadui, akasema mwenyewe “kuwa na silaha “maombi, bidii kwa ajili ya Kristo, na tumaini katika usaada wake.” “Nimejazwa vilevile na upendo wa Mungu na jirani wangu katika moyo wangu, na Biblia inakuwa mikononi mwangu.” “Nilisikia nguvu zangu kuwa ndani ya Kitabu hiki, na kwamba uwezo wake utanilinda.”TSHM 173.1

    Akavumilia mpaka wakati ujumbe ungeweza kupelekwa katika sehemu kubwa ya ulimwengu inayo katiwa na watu. Miongoni mwa Wayahudi, Turks, Parsis, Wahindi, na mataifa na makabila akagawanya Neno la Mungu katika lugha mbalimbali, na mahali po pote akatangaza kukaribia kwa kuja kwa Masiya.TSHM 173.2

    Katika safari yake huko Boukhari akakutana mafundisho ya kurudi kwa Bwana yakifundishwa na watu waliokaa peke yao. Waarabu wa Yemen, akasema, wanakuwa na kitabu kinachoitwa Seera, ambacho kina tangazo la kuja kwa Kristo mara ya pili na ufalme wake wa utukufu; na wanatazamia mambo makuu kutendeka katika mwaka 1840.” “Nikakuta wana wa Israeli, wa kabila la Dani, ... wanaotazamia, pamoja na wana wa Rekabu, kufika kwa upesi kwa Masiya katika mawingu ya mbingu.”TSHM 173.3

    Imani ya namna moja ilipatikana kwa mjumbe mwengine katika Tartares. Padri mmoja wa Tartares akauiiza wakati gani Kristo angekuja mara ya pili. Wakati mjumbe (missionaire) alijibu, kwamba hakujua kitu kwa jambo lile, padri akashangaa kwa ujinga wa namna ile kwa mwalimu wa Biblia, na akaeleza habari ya imani yake mwenyewe, yeye msingi kwa unabii, kwamba Kristo angekuja karibu mwaka 1844.TSHM 173.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents