Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  “Tazama, Bwana Arusi Anakuja”

  Kuja kwa Kristo kama Kuhani Mkuu kwa Pahali patakatifu pa patakatifu kwa usafisho wa Pahali patakatifu (Danieli 8:14), kuja kwa Mwana wa watu kwa Mzee wa Siku (Danieli 7:13), na kuja kwa Bwana katika hekalu yake (Malaki 3:11) ni matukio ya namna moja. Jambo hili pia ni mfano wa kuja kwa bwana arusi kwa ndoa katika mfano wa mabikira kumi wa Matayo 25.TSHM 205.1

  Katika mfano, wakati bwana arusi alipofika, “nao waliokuwa tayari waliingia pamoja naye kwa arusi.” Kuja huku kwa bwana arusi kulifanyika mbele ya arusi. Arusi ni mfano wa kupokelewa na Kristo katika ufalme wake. Mji Mtakatifu, Yerusalema Mpya, mji mkubwa (capitale) ambao ni mfano wa ufalme, unaitwa “bibi arusi, mke wa Mwana-kondoo.” Akasema malaika kwa Yoane: “Kuja hapa, nami nitakuonyesha yule bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.” “Akanichukua katika roho,“nabii asema, “akanionyesha ule mji mkubwa, Yerusalema mtakatifu, ukishuka toka mbinguni, kwa Mungu.” Ufunuo 21:9,10.TSHM 205.2

  Bibi-arusi ni mfano wa Mji Mtakatifu, na mabikira waliotoka kukutana na bwana arusi ni mfano wa kanisa. Katika Ufunuo watu wa Mungu wanaitwa wageni kwa chakula cha arusi. Kama wageni, hawawezi kuwa bibi-arusi. Kristo atapokea kutoka kwa Mzee wa Siku katika mbingu “mamlaka, na utukufu, na ufalme.” Yerusalema Mpya, mji mkubwa wa ufalme wake, “umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mme wake.” Anapokwisha kupokea ufalme, atakuja kama Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana kwa ajili ya ukombozi wa watu wake watakaoshiriki kwa chakula cha arusi ya Mwana-Kondoo. Danieli 7:14; Ufunuo 21:2.TSHM 205.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents