Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mapatano na Ukubali

  Waprotestanti wamesaidia ama kupendelea mafundisho ya Kanisa la Papa; wamefanya mapatano na mkubaliano ambayo wakatoliki wenyewe wameshangaa kuyaona. Watu wanafunga macho yao kwa tabia ya kamili ya Kanisa la Roma. Watu wanahitaji kupinga maendeleo ya adui huyu wa hatari kwa uhuru wa watu na dini.TSHM 276.1

  Wakati msingi wa kanisa la Roma linaimarishwa juu ya madanganyo, si la ushenzi na ujiinga. Huduma ya dini ya Kanisa la Roma kawaida ni ya kuvuta sana. Maonyesho yake mazuri sana mengi na kanuni kubwa za dini zinavuta watu na kunyamazisha sauti ya akili na zamiri. Jicho linavutwa kwa uzuri. Makanisa mazuri kabisa, maandamano makubwa ya ajabu, mazabahu ya zahabu, sanduku za kuwekea vitu vitakatifu za johari, mapicha mazuri, na muchoro bora vinavuta wenye kupenda uzuri. Muziki ni waajabu. Nukta za muziki nzuri za kutoka kwa sauti kubwa za kinanda zinachanganyika na nyimbo tamu sana za sauti nyingi kama inavyoongeza katika madari ya nyumba ya juu sana na sehemu ndefu ya nguzo ya majengo makubwa ya kanisa yake, yanavuta akili ya uchai na heshima.TSHM 276.2

  Utukufu huu wa inje na ibada vinacheka tamaa za nafsi yenye kugonjwa ya zambi. Dini ya Kristo haihitaji mivuto ya namna hiyo. Nuru inayongaa kutoka kwa msalaba inaonekana safi na ya kupendeza na hakuna mapambo ya inje yanayoweza kuongeza damani yake ya kweli.TSHM 276.3

  Mawazo ya juu ya ufundi, malezi ya kupendeza tamaa, mara kwa mara yanatumiwa na Shetani kuongoza watu kusahau mahitaji ya nafsi na kuishi kwa ajili ya ulimwengu huu tu.TSHM 276.4

  Fahari na sherehe ya kuabudu kwa Kikatoliki kunakuwa na uwezo wa kuvuta (kushawishi) kufanya mabaya, nzuri wakupoteza akili, na hiyo, wengi wamedanganyika. Wanajipatia uhakikisho juu ya Kanisa la Roma kuwa mlango wa mbinguni. Hakuna hata mmoja ila tu wale wanaoweka miguu yao kwa msingi wa kweli, ambao mioyo yao hufanywa upya kwa Roho ya Mungu, wanakuwa salama juu ya mvuto wake. Mfano wa utawa pasipo uwezo ni kitu kile wengi wanatamani.TSHM 276.5

  Madai ya Kanisa kwa haki kwa ya kusamehe zambi yanaongoza wafuasi wa Roma kujisikia huru kwa zambi, na agizo la maungamo linaelekea vile vile kutoa ruhusa kwa uovu. Yeye anayepiga magoti mbele ya mtu aliyeanguka na anafungua katika maungamo mawazo ya siri ya moyo wake anapoteza cheo cha nafsi yake. Katika kufunua zambi za maisha yake kwa padri--mwenye kufa wa kosa-cheo cha tabia yake ni chini, na anakuwa mchafu kwa hiyo. Mawazo yake juu ya Mungu ni ya kushusha cheo katika mfano wa mwanadamu aliyeanguka, kwa sababu kuhani anasimama kama mjumbe wa Mungu. Ungamo hili la haya la mtu kwa mtu ni chemchemi ya siri ambamo kumebubujika uwingi wa uovu unaochafua ulimwengu. Kwani kwa yeye anayependa anasa, ni kupendeza zaidi kuungama kwa mtu wa mauti kuliko kufungua roho kwa Mungu. Ni jambo la kupendeza zaidi kwa kiumbe mwanadamu kutubu kuliko kuacha zambi; ni rahisi kuhuzunisha wala kutesa mwili kwa nguo ya gunia kuliko kusulubisha tamaa za mwili.TSHM 277.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents