Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Shetani Ameshindwa

  Kama vile katika bumbuanzi waovu wanatazama ibada ya kuvikwa kwa taji kwa Mwana wa Mungu. Wanaona mikononi mwake mbao za sheria ya Mungu walizozizarau. Wanashuhudia nguvu ya ibada kutoka kwa waliookolewa; na kama wimbi la sauti za nyimbo zinapoenea kwa makutano inje ya mji, wote wanapaaza sauti, “Haki na kweli ndizo njia zako, wewe Mfalme wa watakatifu”. Ufunuo 15:3. Kwa kuanguka na kumusujudu, wakamuabudu mfalme wa uzima.TSHM 327.1

  Shetani anaonekana kama anahangaika. Mara kerubi wa kufunika, anakumbuka mahali gani ameanguka. Kutoka kwa baraza pahali alipoheshimiwa zamani ameondolewa milele. Anaona sasa mwingine anayesimama karibu ya Baba, malaika wa umbo lenye utukufu. Anajua ya kwamba cheo cha malaika huyu kingeweza kuwa chake.TSHM 327.2

  Ufahamu unakumbuka makao ya hali yake ya usafi, amani na kutoshelewa ilivyokuwa yake mpaka wakati wa uasi wake. Anakumbuka kazi yake miongoni mwa watu na matokeo yake--uadui wa mtu kwa watu wenzake, maangamizi ya kutisha ya maisha, kupinduka kwa viti vya enzi, makelele, vita, na mapinduzi. Anakumbuka bidii zake za daima kwa kupinga kazi ya Kristo. Anapoangalia matunda ya kazi yake anaona tu kushindwa. Mara kwa mara katika maedeleo ya vita kuu amekuwa akishindwa na kulazimishwa kuacha.TSHM 327.3

  Kusudi la muasi mkuu lilikuwa daima kuhakikisha kuwa serkali ya Mungu ndiyo msimamizi wa uasi. Ameongoza makundi mengi kukubali maelezo yake. Kwa maelfu ya miaka mkuu huyu wa mapatano ya kufanya mabaya ameficha uwongo kuwa haki. Lakini wakati umefika sasa wakati historia na tabia ya Shetani zitakapofunuliwa. Katika juhudi yake ya mwisho kwa kuondoa Kristo kwa kiti cha enzi, kuharibu watu Wake, na kukamata makao ya Mji wa Mungu, mshawishi mkubwa amekwisha kufunuliwa kabisa. Wale waliojiunga naye wanaona kushindwa kabisa kwa kazi yake.TSHM 327.4

  Shetani anaona ya kwamba uasi wake wa mapenzi haukumstahilisha kuingia mbinguni. Amezoeza nguvu zake kwa vita kumpinga Mungu; usafi na umoja wa mbinguni ungekuwa kwake mateso makubwa. Anainama chini na kukubali haki ya hukumu yake.TSHM 327.5

  Kila swali la kweli na kosa katika mashindano ya siku nyingi limefanywa wazi sasa. Matokeo ya kuweka pembeni sheria za Mungu yamewekwa wazi mbele ya macho ya viumbe vyote. Historia ya zambi itasimama milele kwa wote kama ushuhuda ya kwamba pamoja na kuwako kwa sheria ya Mungu kunafungwa furaha ya viumbe vyote alivyoviumba. Viumbe vyote, vya uaminifu na vyenye uasi, kwa mapatano pamoja vinatangaza, “Haki na kweli njia zako, wewe Mfalme wa watakatifu”.TSHM 327.6

  Saa imefika wakati Kristo anapashwa kutukuzwa juu ya kila jina linalotajwa. Kwa ajili ya furaha inayowekwa mbele yake--ya kwamba aliweza kuleta wana wengi katika utukufu--akavumilia msalaba. Anaangalia kwa waliookolewa, waliofanywa upya kwa mfano wake mwenyewe. Anatazama ndani yao matokeo ya kazi ya roho yake, na anatoshelewa. Isaya 53:11. Kwa sauti ambayo inawafikia makutano, wenye haki na waovu, anatangaza: “Tazama biashara wa damu yangu! Kwa ajili ya hawa niliteseka, kwa ajili ya hawa nilikufa”.TSHM 328.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents