Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tangu Sasa Hata Milele - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Roma Inakusudia Kuangamiza Wavaudois (Waldenses)

    Sasa mapigano makali kuliko yote juu ya watu wa Mungu yakaanza katika makao yao milimani. Wapelelezi (quisiteurs) waliwekwa kwa nyayo yao. Tena na tena mashamba yao yaliyokuwa na baraka yakaharibiwa, makao yao na makanisa madogo yao yakaondolewa. Hakuna mashitaka iliyoweza kuletwa juu ya tabia njema ya namna hii ya watu waliokatazwa. Kosa lao kubwa lilikuwa kwamba hawakuabudu Mungu kufuatana na mapenzi ya Papa. Kwa ajili ya “kosa hili” kila tukano na mateso ambayo watu ao Shetani waliweza kufanya yaliwekwa juu yao.TSHM 28.2

    Wakati Roma ilikusudia kukomesha dini hii (secte) iliyochukiwa, tangazo likatolewa na Papa kuwahukumu kama wapingaji wa dini na kuwatoa kwa mauaji. (Tazama Nyongezo). Hawakusitakiwa kama wavivu, wasio waaminifu, ao wasio na utaratibu; lakini ilitangazwa kwamba walikuwa wenye mfano wa wenye utawa na utakatifu uliovuta “kondoo la zizi la kweli”. Tangazo hili likaita washiriki wote wa kanisa kuungana kwa mapigano yawapingaji wa dini Kama vile kuchochea tangazo hili liliachia viapo vyovyote wote waliokubali kwenda kwa vita; tangazo hili likawatolea haki kwa kila mali waliweza kupata kwa wizi, nalika ahidi ondoleo la zambi zote kwa yule angeweza kuua mpinga dini yeyote. Jambo hilo likavunja mapatano yote yaliyofanywa kwa upendeleo wa Wavaudois, wakakataza watu wote kuwapa msaada wowote, na kuwapa uwezo watu wote kukamata mali yao”. Andiko hii linafunua wazi wazi mungurumo wa joka, na si sauti ya Kristo. Roho ya namna moja iliyosulibisha Kristo na kuua mitume, ile ilisukuma Nero mwenye hamu ya kumwaga damu juu ya waaminifu katika siku zake, ilikuwa kazini kwa kuondoa juu ya dunia ya wale waliokuwa wapendwa wa Mungu.TSHM 28.3

    Bila kutazama vita ya Papa juu yao na mauaji makali sana waliyoyapata, watu hawa wanaogopa Mungu waliendelea kutuma wajumbe (Missionnaires) kutawanya ukweli wa damani. Waliwindwa hata kuuwawa, lakini damu yao ilinywesha mbegu iliyopandwa na kuzaa matunda.TSHM 28.4

    Kwa hivyo Wavaudois walishuhudia Mungu kwa karne nyingi kabla ya Luther. Walipanda mbegu ya Matengenezo (Reformation) yale yaliyoanza wakati wa Wycliffe, yakaota na kukomaa katika siku za Luther, na yanapaswa kuendelea hata mwisho wa wakati.TSHM 29.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents