Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Cheti cha Usalama cha Luther Katika Hatari

  Wajumbe wa Papa tena wakaagiza kwamba hati ya kupita salama ya Mtengenezaji isiheshimiwe. “Rhine (jina la mto) unapashwa kupokea majivu yake, kama ulivyopokea yale majivu ya John Huss kwa karne iliyopita.” Lakini watawala wa Ujeremani, ingawa walijitangaza kuwa adui kwa Luther, wakakataa kuvunja ahadi iliotolewa mbele ya taifa. Wakataja misiba ambayo iliyofuata kifo cha Huss. Hawakusubutu kuleta juu ya Ujeremani maovu makali mengine.TSHM 74.1

  Charles, kwa kujibu kwa shauri mbaya, akasema: “Ijapo heshima na imani ingepaswa kufutwa mbali ulimwenguni mwote, vinapaswa kupata kimbilio ndani ya mioyo ya wafalme.” Akalazimishwa na maadui wa Luther wa kipapa kumtendea Mtengenezaji kama vile Sigismund alivyomtendea Huss. Lakini akakumbuka Huss alipoonyesha minyororo yake kati ya makutano na kumkumbusha mfalme juu ya imani yake aliyoahidi, Charles V akasema, “Singetaka kufazaika kama Sigismund.”TSHM 74.2

  Lakini kwa kusudi tu Charles akakataa ukweli uliotolewa na Luther. Alikataa kuacha njia ya desturi kwa kutembea katika njia za kweli na haki. Kama baba zake, alitaka kupigania dini ya Papa. Kwa hiyo akakataa kukubali nuru mbele ya wazazi wake.TSHM 74.3

  Kwa siku zetu, kuna wengi wanaoshikilia desturi za asili za mababa zao. Wakati Bwana anapotuma nuru mpya wanakataa kuipokea kwa sababu haikupokelewa na wababa wao. Hatutakubaliwa na Mungu tunapotazama kwa wababa wetu kwa kuamua wajibu wetu pahali pa kutafuta Neno la Kweli kwa ajili yetu wenyewe. Tutaulizwa juu ya nuru mpya inayoangaza sasa juu yetu kutoka kwa Neno la Mungu.TSHM 74.4

  Uwezo wa Mungu ulisema kupitia Luther kwa mfalme na watawala wa Ujeremani. Roho yake iliwasihi kwa mara ya mwisho kwa wengi katika mkutano ule. Kama Pilato, karne nyingi mbele yao, kama vile Charles V, katika kujitoa kwa jeuri ya ulimwengu, akaamua kukana nuru ya ukweli.TSHM 74.5

  Mashauri juu ya Luther yakaenea pote, yakaleta wasiwasi katika mji wote. Rafiki wengi, walipojua ukali wa hila ya Roma, wakakusudia kwamba Mtengenezaji hakupaswa kutolewa kafara. Mamia ya wenye cheo wakaahidi kumlinda. Kwa milango ya nyumba na katika pahali pa watu wote matangazo ya kubandikwa ukutani yakawekwa, mengine yalikuwa yakuhukumu na mengine ya kumkubali Luther. Kwa tangazo moja kukaandikwa maneno ya maana, “Ole wako, Ee inchi, wakati mfalme wako ni mtoto.” Muhubiri 10:16. Furaha nyingi kwa ajili ya Luther ikasadikisha mfalme na baraza kwamba kila jambo lisilo la haki lililoonyeshwa kwake lingehatarisha amani ya ufalme na nguvu ya kiti cha mfalme.TSHM 75.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents