Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uponyaji Unaweza Kutoka kwa Shetani, Sura ya 140

    “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.” 1 Petro 5:8.Mar 148.1

    Dhana potofu za Shetani sasa zinazidi kuongezeka, na wale ambao wanachepuka na kuiacha njia ya kweli watapoteza uthabiti wao. Wakiwa hawana kitu cha kuwashikilia, watahama kutoka udanganyifu mmoja hadi mwingine, huku wakipeperushwa na pepo za mafundisho mageni. Shetani ameshuka akiwa na uwezo mwingi. Wengi watadanganyika kwa miujiza yake.Mar 148.2

    Nimeagizwa kusema kuwa katika siku za usoni, uangalifu mkubwa sana utahitajika. Hali ya ujinga wa kiroho haipaswi kuwapo miongoni mwa watu wa Mungu. Pepo wabaya wanafanya bidii ili wapate kutawala akili za wanadamu. Watu wanajikusanya vitita vitita, tayari kwa kuchomwa na myoto ya siku za mwisho. Wale ambao wanamkataa Kristo na haki yake watapokea madanganyo ambayo yanaelekea kuifunika dunia yote. Wakristo hawana budi wawe na kiasi na kukesha, wakimpinga adui Shetani kwa uthabiti, ambaye kama simba angurumaye, anazunguka zunguka akitafuta mtu ammeze. Chini ya uwezo wa pepo wabaya, watu watatenda miujiza. . .Mar 148.3

    Hatuna sababu ya kudanganyika. Matukio ya ajabu, ambayo Shetani atahusika nayo kwa karibu sana, yatatukia hivi karibuni. Neno la Mungu linatamka kwamba Shetani atafanya miujiza. Atawafanya watu waugue, na kisha atawaondolea nguvu zake za kishetani. Na hivyo watafikiriwa kuwa wameponywa. Matendo haya ambayo yataonekana kama uponyaji halisi, yatawajaribu Waadventista wa Sabato ...Mar 148.4

    Ikiwa wale ambao uponyaji huu linafanyika kupitia kwao wataelekea kutoa udhuru kwa kutojali kwao sheria ya Mungu, na wakaendelea katika uasi, basi, hata kama wangekuwa na uwezo wa kiwango cho chote kile, hiyo haina maana kwamba wana uwezo mkuu wa Mungu. Kinyume chake, huo ni uwezo utendao miujiza wa yule mdanganyifu mkuu. Yeye ni mwasi wa ile sheria ya maadili, naye anatumia kila mbinu anayoweza kuisimamia, ili kuwapofusha watu wasiifahamu tabia yake halisi. Tumeonywa kuwa katika siku za mwislio, Shetani atafanya kazi kwa ishara na ajabu za uongo. Naye ataendelea kufanya maajabu hayo mpaka wakati wa kufungwa kwa mlango wa rehema, ili apate kuwaelekeza watu kwenye maajabu hayo kama ushahidi kwamba yeye ni malaika wa nuru na siyo wa giza.Mar 148.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents