Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Matokeo ya Maono ya Uongo, Sura ya 150

    Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.” Mathayo 7:19, 20.Mar 158.1

    Watu kadhaa wanaoishi sasa (1890) ni wenye mashaka, hawaamini katika vipawa vya kanisa, hawana imani na ukweli, na hawana dini kabisa. Nilioneshwa kwamba hao ni matokeo ya hakika ya maono ya uongo . . .Mar 158.2

    Daima Shetani anakazana kuleta uongo ili kuwaondoa watu katika kweli . . .Mar 158.3

    Udanganyifu wa mwisho kabisa wa Shetani utakuwa ni kuzifanya shuhuda za Roho wa Mungu zisiwe na manufaa yo yote. “Pasipo maono, watu huacha kujizuia” (Mit. 29:18). Shetani atafanya kazi kwa werevu sana, kwa namna nyingi na kupitia mawakala mbalimbali ili kuvuruga imani ya watu wa Mungu wa masalio katika shuhuda za kweli. Ataleta maono ya uongo ili kupotosha, naye atachanganya ukweli na uongo na kuwachukiza sana watu kiasi kwamba watachukulia kuwa kila kitu chenye jina la maono ni aina fulani ya ushupavu wa dini; lakini kwa kulinganisha na kutofautisha ukweli na uongo, wale ambao ni waaminifu watawezeshwa kupambanua kati ya ukweli na uongo ...Mar 158.4

    Hakuna kitu kilicho na madhara sana kwa hali njema ya roho, usafi wake, ufahamu mtakatifu na wa kweli juu ya Mungu, na mambo matakatifu na ya milele, kuliko kusikiliza na kuyatukuza daima mambo ambayo hayatoki kwa Mungu. Kunauchafua moyo na kudhoofisha ufahamu. Kutokana na mvuto wake unaoadilisha, unaosafisha na kutakasa tabia ya mpokeaji, ukweli mkamilifu unaweza kufuatiliwa hadi katika Chanzo chake kitakatifu. Mwanzilishi wa ukweli wote aliomba hivi kwa Baba yake, “Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma” (Yohana 17:20, 21).Mar 158.5

    Mambo yatakuwa yanainuka daima ili kuleta mgawanyiko na kuwavuta watu kutoka kwenye kweli. Kuonea mashaka ukweli, ukosoaji, kushutumu, na kuwahukumu wengine, sio ushahidi wa neema ya Kristo moyoni. Hakuleti umoja. Wakati uliopita, kazi kama hiyo iliwahi kufanywa na watu waliodai kuwa na nuru ya ajabu, huku wakiwa wamezama dhambini.Mar 158.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents