Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuingia Mstarini, Sura ya 151

    Walioonewa watakapoona watafurahi; Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.” Zaburi 69:32.Mar 159.1

    Ni fursa yako kuwa na furaha katika BWANA, na kushangilia katika maarifa ya neema yake inayotutunza. Hebu upendo wake utawale akili na moyo yako. Chunga dhidi ya uchovu, uzembe, fadhaa. Toa ushuhuda wenye kutia moyo. Ondoa macho yako toka kwa kile kilicho giza na cha kukatisha tamaa, kisha mtazame Yesu, Kiongozi wetu mkuu, ambaye chini ya uangalizi wake mwema mpango wa ukweli wa leo, ambao kwa huo tunatoa maisha yetu na vyote, umekusudiwa kushinda kwa utukufu mkuu. . . .Mar 159.2

    Hebu ionekane . . . kwamba Yesu anafanya makazi moyoni, akitunza, akiimarisha, akifariji. Ni fursa yako kujazwa, siku kwa siku, kwa uwezo maridhawa wa Roho Mtakatifu na kuwa na mtazamo mpana wa umuhimu na upeo wa ujumbe tunaouhubiri ulimwenguni. BWANA yuko tayari kukufunulia mambo ya ajabu katika sheria yake. Mngojee kwa moyo wa unyenyekevu. Omba upate kuelewa nyakati tunazoishi ndani yake, ili kuelewa kikamilifu kusudi lake, na kuongezewa ufanisi zaidi katika uongoaji roho. . . .Mar 159.3

    Ni vyema kwetu kutafakari kile kilicho mbioni kuupata ulimwengu. Huu siyo wakati wa uzembe au kujinufaisha nafsi. Endapo nyakati tunazoishi zitashindwa kugusa akili zetu, ni kitu gani tena kitatugusa?. . .Mar 159.4

    Watu walio wepesi katika kuelewa mambo wanahitajika sasa. Mungu anawaita wale walio tayari kuongozwa na Roho Mtakatifu kupiga hatua katika kazi njema ya matengenezo. Naona zahama mbele yetu, naye BWANA anawaita wafanyakazi wake waingie kazini. Kila roho yapaswa kujitoa wakfu kwa Mungu kwa dhati kuliko ilivyokuwa miaka iliyopita. . . .Mar 159.5

    Niliguswa sana na mambo niliyooneshwa hivi karibuni wakati wa usiku. Kulionekana kuwepo vuguvugu kubwa—kazi ya matengenezo—ikisonga mbele katika mahali mbalimbali. Watu wetu walikuwa wanaingia kazini, wakiitikia wito wa Mungu Je hatutatii sauti yake? Je hatutarekebisha taa zetu, na kuenenda kama watu watarajiao kurudi kwa BWANA? Huu ni wakati wa kutangaza nuru, ni wakati wa kuchukua hatua.Mar 159.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents