Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Matukio ya Siku za Mwisho Yamefunuliwa Wazi, Sura ya 152

    Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake. Amosi 3:7Mar 160.1

    Matukio yanayohusiana na ufungwaji wa mlango wa rehema na kazi ya maandalizi kwa wakati wa taabu yamefunuliwa kwangu. Lakini watu wengi hawafahamu kweli hizi muhimu kana kwamba kamwe hazijawahi kufunuliwa. Shetani anatafuta kufutilia mbali kila mwelekeo wenye kuleta hekima ya wokovu, na wakati wa taabu utawakuta hawako tayari.Mar 160.2

    Kadri tunavyokaribia kufungwa kwa historia ya ulimwengu huu, unabii unaohusiana na siku za mwisho kwa namna maalumu unahitaji tupate kuujifunza kwa makini. Kitabu cha mwisho cha maandiko ya Agano Jipya kimejaa ukweli tunaohitajika kuujua kwa kina.Mar 160.3

    Ujumbe wa onyo uliotolewa kwa mpangilio maalumu katika kitabu cha Ufunuo wapaswa kuchukua nafasi ya kwanza akilini mwa watu wa Mungu. . . . Muda wa thamani unapita kwa kasi na ipo hatari kwamba wengi watapokonywa muda wao mteule ambao wangaliutumia kutangaza ujumbe ambao Mungu ameutuma kwa dunia iliyoasi. Shetani anafurahi kuona mioyo iliyotanga mbali kimawazo iache jukumu lake la kujifunza ukweli unaohusu mambo ya umilele.Mar 160.4

    Ushuhuda wa Kristo, ushuhuda wa hadhi kuu kiroho, wapaswa kutolewa kwa ulimwengu. Pote katika kitabu cha Ufunuo zipo ahadi za thamani, zenye kuleta matumaini, na pia yapo maonyo yenye umuhimu mkuu. Je wale wanaokiri kuwa na maarifa ya kweli hawapaswi kusoma ushuhuda Yohana aliopatiwa na Kristo? Hapa hakuna kubahatisha, hakuna ulaghai wa kisayansi. Hapa ni ukweli unaohusu maslahi yetu ya sasa na ya umilele. Makapi ni yapi na ngano ni ipi?Mar 160.5

    Ni wale tu ambao wamekuwa wanafunzi waaminifu wa Maandiko na ambao wamepokea upendo wa ile kweli watakaohifadhiwa dhidi ya udanganyifu mkuu unaoukumba ulimwengu. Kupitia ushuhuda wa Biblia tutamgundua mlaghai ajaye kwa kificho. Kwa wote muda wa kujaribiwa utawasili. Kwa kupepetwa kupitia majaribu Mkristo wa kweli atajulikana. Je watu wa Mungu kwa sasa wamesimikwa kikamilifu katika Neno lake kiasi kwamba hawatafuata mivuto ya hisia zao? Je wao, katika zahama hiyo, watadumu kushikilia Biblia na Biblia pekee?Mar 160.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents