Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mikakati ya Shetani Dhidi ya Washikao Sabato, Sura ya 155

    “Je cha udhalimu kishirikiane nawe, Kitungacho madhara kwa njia ya sheria? Huishambulia nafsi yake mwenye haki, na kuihukumu damu isiyo na hatia.” Zaburi 94:20,21.Mar 163.1

    Kadri watu wa Mungu wanavyokaribia hatari za siku za mwisho, Shetani anafanya na malaika zake kutafuta mpango kabambe wa kupindua imani yao. . .Mar 163.2

    Shetani mdanganyifu mkuu asema: “... Sabato ndilo jambo litakaloamua mustakabali wa roho. Hebu tuinue juu sabato yetu tuliyojiundia. Tumesababisha watu wa dunia na washiriki wa kanisa waipokee; sasa kanisa linapaswa kushawishiwa liunge mkono dunia katika kuiadhimisha sabato yetu bandia. Twapaswa kutenda kazi kwa ishara na miujiza kuwapofusha macho yao wasiujue ukweli, na kuwaongoza kuondolea mbali akili na hofu ya Mungu wavutwe kufuata desturi na mapokeo.Mar 163.3

    “Nitawashawishi wachungaji mashuhuri kuelekeza usikivu wa wasikilizaji wao nje ya amri za Mungu. . .Mar 163.4

    “Lengo letu la msingi ni kuwanyamazisha kundi la washika Sabato. Sharti tusababishe watu wapate kuwachukia. Tutasajili watu mashuhuri wenye hekima wawe upande wetu, na kuwashawishi walio katika mamlaka kutekeleza makusudi yetu. Ndipo sabato niliyoianzisha itashurutishwa kwa sheria kali za kutisha. Wale wanaozipuuza watafukuzwa watoke mjini na vijijini, wateseke kwa njaa na maisha magumu. Mara tupatapo mamlaka, tutaonyesha lile tuwezalo kutenda kwa wale wasiotaka kuachana na utii wao kwa Mungu. . . . Sasa maadamu tunayaleta pamoja makanisa ya Kiprotestanti na dunia na yanakubaliana na mkono wetu wa kulia wa uweza, hatimaye tutakuwa na sheria ya kuteketeza wote ambao hawatajisalimisha kwa mamlaka yetu. Pale kifo itapokuwa adhabu ya kuwapatia wote wanaoiasi sabato yetu, basi wengi wasio na ushirika na washika Sabato ya kweli ya Mungu watahamia upande wetu.Mar 163.5

    “Lakini kabla hatujaingia katika utekelezaji wa hatua hizi ngumu za kutisha, sharti . . . tuwe na mbinu ya kuwalaghai tuwanase wale wenye kuheshimu Sabato ya kweli. Twaweza kuwatenga wengi mbali na Kristo kupitia anasa, tamaa, na kiburi. Wanaweza kujidhania wenyewe kwamba wako salama kwa vile wanausadiki ukweli, ila uzamaji katika uchu na tamaa mbaya, zenye kuchanganya maamuzi, na kuharibu uwezo wa upambanuaji, utawasababisha waanguke.”Mar 163.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents