Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Namna Sanamu ya Mnyama Inavyojitokeza, Sura ya 161

    “Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.” Ufunuo 13:12.Mar 169.1

    Ili Marekani ipate kulinda sanamu ya mnyama, nguvu za kidini sharti zitawale serikali ya kiraia kiasi kwamba mamlaka ya taifa yatatumiwa pia na kanisa kukamilisha malengo yake binafsi. . . .Mar 169.2

    “Sanamu ya mnyama” inawakilisha namna ile ya Uprotestanti ulioasi ambao utakuzwa wakati makanisa ya Kiprotestanti yatakapotafuta msaada wa nguvu za kiserikali ili kushurutisha mfumo wa imani yao ya kidini. . . .Mar 169.3

    Wakati uadhimishaji Jumapili utashurutishwa kupitia sheria za nchi, na ulimwengu utaangaziwa nuru utambue wajibu wake kuitii Sabato ya kweli, ndipo pale kila atakayekaidi amri ya Mungu, akatii maagizo ambayo hayana mamlaka ya juu kuliko ile ya Rumi, watakuwa wameheshimu upapa zaidi ya kumtii Mungu. Atakuwa anaheshimu Rumi na mamlaka yenye kushurutisha asasi iliyoanzishwa na Rumi. Atakuwa anaabudu mnyama na sanamu yake. Kadri wanadamu wanavyoikataa asasi ambayo Mungu ameianzisha na kutangaza kuwa iwe ishara ya mamlaka yake, na badala yake kuheshimu kile ambacho Rumi imekichagua kama ishara ya ukuu wake, kwa jinsi hiyo watakuwa wamepokea dalili ya utii kwa Rumi--“alama ya mnyama.” Na ni hadi hapo suala linalohusika limewekwa wazi mbele za watu, nao wameongozwa kuchagua kati amri za Mungu na maagizo ya wanadamu, na kwamba wale watakoendelea katika uasi watapokea “alama ya mnyama.”Mar 169.4

    Katika suala linaloshindaniwa Ukristo utagawanyika katika makundi mawili mkuu—wale wanaotunza Amri za Mungu na imani ya Yesu, na wale wanaomwabudu mnyama na sanamu yake na kupokea alama yake. Japo kanisa na serikali wataunganisha nguvu zao kushurutisha “wote, wadogo kwa wakubwa na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa” (Ufu. 13:16), wapokee “alama ya mnyama,” ila watu wa Mungu hawataipokea. Nabii wa Patmo anawaona “wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kandokando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu. Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi, Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa. Ufu. 15:2, 3.Mar 169.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents