Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Suala la Sabato Dhidi ya Jumapili, Sura ya 164

    “Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-kondoo.” Ufunuo 14:9, 10.Mar 172.1

    Kabla ya hapa wale ambao wamekuwa wakiwasilisha ujumbe wa malaika yule wa tatu wamekuwa wakionekana kama wanaoshtua watu kwa kelele zisizo za lazima. Utabiri wao kwamba kukosa ustamilivu katika suala la dini kungetawala Marekani, na kwamba kanisa na serikali vingeungana kuwatesa wale wazishikao amri za Mungu, umeitwa kuwa usio na msingi na wa kipuuzi . . . Lakini wakati suala la kutekeleza sheria ya kuiadhimisha Jumapili linapozidi kusikika, tukio ambalo limekuwa likitiliwa mashaka kwa muda mrefu na kutokuaminika linaonekana likikaribia, na ujumbe wa malaika yule wa tatu utaweka matokeo ambayo yasingepatikana kabla ya wakati huo.Mar 172.2

    Watu wa imani na maombi watalazimika kusonga mbele wakiwa na ari takatifu, huku wakitangaza maneno wanayopewa na Mungu. Dhambi za Babeli zitawekwa wazi. Matokeo ya kutisha ya mamlaka za watu kushinikiza kuadhimisha mambo ya kanisa, ambayo ni namna za kuingiliwa na umizimu, maendeleoya kificho lakini yenye haraka ya mamlaka ya upapa -yote yatawekwa wazi. Maonyo haya mazito yatawaamsha watu .... Watu watakapokwenda kwa waalimu wao wa zamani na kuwauliza kwa shauku; “Je, mambo haya ndivyo yalivyo?” Wachungaji watawasilisha hadithi, watatabiri mambo laini, ili kutuliza hofu na kunyamazisha dhamiri zao zilizoamka. Lakini kwa sababu wengi watakataa kuridhishwa na mamlaka ya watu na hivyo kudai “kile asemacho Bwana,” jumuiya ya kidini inayopendwa, kama walivyokuwa Mafarisayo wa zamani, hali wakiwa wamejazwa na ghadhabu kwa sababu ya mamlaka yao kutiliwa mashaka, wataukataa ukweli na kuuita kuwa wa Shetani na hivyo kuwaamsha makutano wapendao dhambi ili wawalaani na kuwatesa wale wanaoutangaza ukweli.Mar 172.3

    Wakati pambano linapoendelea hadi kufikia maeneo mapya na mawazo ya watu yanapoitwa kwa sheria ya Mungu iliyokanyagwa, Shetani atafanya vurugu. Nguvu iendayo na ujumbe itawaudhi wale wanaoupinga ujumbe huo. Wachungaji watajaribu kutumia kila namna ya jitihada na uwezo walio nao hata kama wangeweza kuzuia nuru kwa kutumia uwezo usio wa kibinadamu ili nuru ising’azwe kwa watu wao. Watajaribu kutumia kila njia itakayokuwa katika uwezo wao ili kuzuia mjadala wa maswali haya muhimu. Kanisa litaalika mkono wa nguvu wa mamlaka ya kiraia na katika kazi hii, upapa na Uprotestanti vitaungana.Mar 172.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents