Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Vielelezo Katika Ujumbe wa Malaika Watatu, Sura ya 165

    “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya.” Malaki 4:5.Mar 173.1

    Ili kuandaa watu wawe tayari kusimama katika siku ya Mungu kazi kubwa ya matengenezo ilipaswa ifanywe [na Waadventista], Mungu aliona kuwa wengi kati ya wale waliodai kuwa watu wake hawakuwa wakijenga kwa ajili ya umilele, na kutokana na rehema yake alikuwa tayari kutuma ujumbe wa onyo ili kuwaamsha toka katika ujinga wao na kuwaongoza katika kujiandaa na ujio wa Bwana.Mar 173.2

    Onyo linawekwa wazi katika Ufunuuo 14. Hapa ndipo ulipo ujumbe uliokuja kwa awamu tatu unaowakilishwa katika lugha ya mahubiri yafanayofanywa na nafsi za mbinguni na mara baada ya hapo kufuatiwa na ujio wa Mwana wa Adamu ili kuvuna “mavuno ya nchi.”Mar 173.3

    Malaika wanawakiIishwa kama warukao katikati ya mbingu, wakiuhubiri ulimwengu ujumbe wa onyo, na ujumbe ukiwa na mguso wa moja kwa moja kwa watu waishio katika siku za mwisho za historia ya dunia hii. Hakuna mtu anayesikia sauti ya malaika hawa, kwani wao wanatajwa hapa kama vielelezo vinavyowakilisha watu wa Mungu wanaotenda kazi kwa mpatano na viumbe wa mbinguni.Mar 173.4

    Ujumbe wa malaika watatu unapaswa uunganishwe, na utoe nuru yake iliyo katika mafungu matatu kwa ulimwengu. Katika kitabu cha Ufunuo, Yohana anasema, “Naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu, na nchi ikaangazwa na utukufu wake.”.. Hii inawakilisha utoaji wa ujumbe wa mwisho unaokuja katika mafungu matatu ukiwa onyo kwa ulimwengu.Mar 173.5

    Ufunuo 18 inaelekeza kwa wakati ambapo, kanisa litakuwa limefikia hali iliyotabiriwa katika ujumbe wa malaika wa pili, kama matokeo ya kukataa onyo linalokuja katika ujumbe wenye sehemu kuu tatu wa Ufunuo 14:6-12. Watu wa Mungu ambao bado wako Babeli wataitwa ili waache kushirikiana nayo. Ujumbe huu ni wa mwisho kabisa kati ya zote zitakazotolewa kwa ulimwengu; na utakamilisha kazi yake. Wakati “wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu” (2 The 2:12), watakapoachwa ili waliamini uongo, ndipo nuru ya kweli itakapong’aa kwa wote ambao mioyo yao ipo tayari kuipokea, na watoto wa Bwana waliosalia Babeli wataitikia wito: “Tokeni kwake, enyi watu wangu.” (Ufu. 18:4).Mar 173.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents