Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Lawama za Maafa kwa Watu wa Mungu, Sura ya 168

    Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu. Ufunuo 12:12.Mar 176.1

    Watu wanapokwenda mbali zaidi na Mungu, Shetani anaruhusiwa kuwa na uwezo wa kuwatawala wana wa kuasi. Anavurumisha maangamizo kwa watu. Kuna maafa katika nchi na bahari. Uhai wa watu unaangamizwa na vitu vinateketezwa kwa moto na mafuriko. Shetani ameamua kuelekeza haya kwa wale wanaokataa kuiinamia sanamu ambayo ameisimamisha. Mawakala wake wataelekeza vidole kwa Waadventista wa Sabato kama chanzo cha matatizo. Watasema, “Watu hawa wamesimama kupinga sheria. Wanainajisi Jumapili. Kama wangelazimishwa kutii sheria ya kushika Jumapili, hizi hukumu za kutisha zingekoma.”Mar 176.2

    Maafa yatakuja - majanga ya kutisha, yasiyotegemewa; na maangamizo haya yatafuatana moja baada ya lingine. Kama kutakuwa na kusikiliza maonyo ambayo Mungu ameyatoa, na kama makanisa yatatubu, na kurejea katika utii kwake, basi majiji mengine yanaweza yasiangamizwe kwa muda. Lakini kama watu ambao wamedanganywa wataendelea katika njia hiyo hiyo ambayo wamekuwa wakiipitia, wakidharau sheria ya Mungu na kuwasilisha uongo kwa watu, Mungu atawaruhusu wapitie majanga, ili hisia zao ziamshwe.Mar 176.3

    Hukumu zitakuja kulingana na uovu wa watu na nuru ya kweli ambayo wameipata. Kama wamekuwa na kweli, wataadhibiwa kulingana na nuru hiyo.Mar 176.4

    Shetani anaweka fasiri zake katika matukio, na watu [wanaoongoza] wanafikiri, kama atakavyo yeye, kuwa maafa yatakayoijaza nchi ni matokeo ya uvunjifu wa Jumapili. Huku wakidhani wanatuliza ghadhabu ya Mungu, watu hawa wenye nafasi kubwa katika jamii watafanya sheria za kushinikiza ushikaji wa Jumapili.Mar 176.5

    Hawa wanadhani kuwa kwa kiliinua siku hii isiyo ya kweli juu na hata juu zaidi, huku wakishurutisha utii wa sheria ya Jumapili, sabato hii ya uongo, wanafanya huduma impendezayo Mungu. Wale wanaomheshimu Mungu kwa kushika Sabato ya kweli wanaangaliwa kama wasiomtii Mungu, wakati ambapo ni wale wengine wanaoitii sheria yao ambao ndio wasiotii, kwa sababu wanaikanyaga Sabato iliyoanzia Eden.Mar 176.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents