Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ishara kwa Ajili ya Kutoka Kwenye Majiji, Sura ya 172

    Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu) ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani. Mathayo 24:15,16.Mar 180.1

    Haitachukua muda mrefu, ambapo, kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa awali, tutalazimika kutafuta kimbilio mahali palipo pweke. Kama jinsi majeshi ya Kirumi yalipozingira Yerusalemu ilikuwa ishara ya kukimbia kwa Wakristo wa Uyahudi, vivyo hivyo, Marekani itakapotumia mamlaka katika tamko la kushinikiza sabato ya upapa itakuwa onyo kwetu. Kwetu basi, huo utakuwa wakati wa kuacha miji mikubwa, ikiwa pia ni maandalizi ya kuondoka kwenye miji midogo na kwenda kwenye nyumba za mapumziko katika maeneo ya upweke milimani.Mar 180.2

    Kwa miaka kadhaa mmekuwa nikipewa nuru maalum ielekezayo kuwa hatupaswi kuweka vituo vya kazi yetu katika majiji. Ghasia na machafuko yanayojaza majiji, hali inayoletwa na jumuiya za wafanyakazi pamoja na migomo, vitakuwa vizuizi vikubwa kwa kazi yetu. Watu wanatafuta kuwakusanya wale wote waliopo katika biashara na shughuli mbalimbali chini ya kongwa la Jumuiya au vyama fulani. Huu siyo mpango wa Mungu, bali mpango wa mamlaka ambayo hatupaswi kuikubali kwa namna yoyote. Neno la Mungu linatosha; waovu wanajifunga pamoja wao wenyewe tayari kwa ajili ya kuchomwa.Mar 180.3

    Vyama vya wafanyakazi na mashirikisho ya kidunia ni mtego. Kaa mbali navyo, tena jitenge navyo, ndugu yangu. Usiwe na lolote na hivyo. Hivi karibuni, itakuwa vigumu sana kwa taasisi zetu kufanya kazi zao katika miji mikubwa kwa sababu ya vyama hivi na mashirikisho haya. . . . Elimisha watu wetu ili watoke kwenye miji mikubwa na waende mashambani, ambapo wanaweza kupata sehemu za ardhi, na pale wanaweza kuwa na nyumba kwa ajili yao wenyewe na watoto wao... Muda si mrefu, kutakuwa na ugomvi na machafuko katika miji mikubwa, kiasi kwamba wale wanaotamani kutoka katika majiji hayo hawataweza.Mar 180.4

    Hatupaswi kujiweka wenyewe mahali ambapo tutalazimishwa kuingia katika mahusiano ya karibu na wale wasiomheshimu Mungu. . . Zahama inakuja hivi karibuni inayohusu uadhimishaji wa siku ya Jumapili.. . .Mar 180.5

    Jumuiya yote inayounga mkono Jumapili inazidi kujipa nguvu katika madai yake ya uongo, na hili litamaanisha mateso kwa wale wanaokusudia kushika Sabato ya Bwana. . .Mar 180.6

    Kulingana na jinsi Mungu anavyotukirimia, kama tunaweza kupata sehemu salama mbali na miji mikubwa, Bwana atafurahi tufanye hili. Nyakati za taabu ziko mbele yetu.Mar 180.7

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents