Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Waaminifu Hawatashindwa, Sura ya 20

    Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu. Ufunuo 14:12.Mar 28.1

    Ni vigumu kulishikilia mwanzo wa imani yetu mpaka mwisho; na ugumu huongezeka kunapokuwa na mivuto ya siri ambayo inaleta roho nyingine kila wakati, nguvu ya upinzani, isimamayo upande wa Shetani katika hoja. Kwa sababu ya kutokuwa na mateso, kuna walioingia miongoni mwetu na kuonekana wanyofu na Ukristo wao hauna mashaka, lakini ambao, kukitokea mateso, wataondoka kwetu. Wakati wa dhiki, wataona nguvu katika hoja potofu zilizokuwa na mvuto katika akili zao. Sheria ya Mungu itakapokataliwa, kanisa la Mungu litapepetwa kwa majaribu makali, na sehemu kubwa kuliko tunayoitegemea kwa sasa, watasikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. Badala ya kuimarika wanapopita katika dhiki, wengi wataonekana kuwa si matawi hai ya Mzabibu wa Kweli. . .Mar 28.2

    Lakini wakati ulimwengu unaikataa sheria ya Mungu, kutakuwa na athari gani kwa wale walio watii kweli na wenye haki? Je, watachukuliwa na wimbi kubwa la uovu? Kwa kuwa watu wengi sana watakuwa wanajiunga chini ya bendera ya mkuu wa giza, watu wanaotii amri za Mungu watayumba kutoka katika utii wao? Hasha! Hakuna hata mmoja atakayekuwa anakaa ndani ya Kristo atakayeanguka. Wafuasi wake watainama na kutii mamlaka ya juu zaidi kuliko ya mtawala ye yote wa duniani. Wakati dharau iliyowekwa juu ya amri za Mungu inawafanya wengi kuutweza ukweli na kutokuuheshimu ipasavyo, wale waaminifu watauinua juu ukweli unaoutofautisha na uongo kwa umakini mkubwa. Hatujaachwa bila kiongozi....Tunapaswa kulisoma neno lake kwa mioyo ya unyenyekevu, kutaka ushauri wake, na kuacha mapenzi yetu na kuyashika ya kwake. Hatuwezi kufanya jambo lo lote bila Mungu.Mar 28.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents