Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uchelewaji kwa Kijiamini na Kutojali, Sura ya 26

    Tazama naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende nchi hata watu wakaione aibu yake. Ufunuo 16:15.Mar 34.1

    Mtumishi mwovu anasema moyoni mwake, “Bwana wangu amechelewa kuja.” Hasemi kwamba Kristo hatakuja. Halifanyii dhihaka wazo la ujio wake wa pili. Lakini katika moyo wake na kwa matendo na maneno yake anatangaza kuwa kuja kwa Bwana kumechelewa Imani ya kwamba Bwana anakuja upesi, anaiondoa katika mioyo ya watu wengine. Ushawishi wake unasababishia watu uchelewaji wa kipuuzi na kutojali. . . Anajichanganya na ulimwengu. . . Hili ni badiliko la hatari katika mtazamo. Anaingia katika mtego pamoja na ulimwengu.Mar 34.2

    “Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.” Ufu. 3:3. Ujio wa Kristo utawashtukiza walimu wa uongo. Watasema, “Amani na salama.” Kama ilivyokuwa kwa makuhani na walimu kabla ya kuanguka kwa Yerusalemu, watakuwa wanatazamia kanisa lifaidi mafanikio na utukufu wa kidunia. Ishara za nyakati watazifasiri kama utangulizi wa jambo hilo. Lakini Bwana wa uvuvio anasema nini? “Ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla.” 1 The. 5:3. Kwa wale wote wanaokaa juu ya uso wa nchi, kwa wale wote walioufanya ulimwengu huu kuwa nyumbani kwao, siku ya Bwana itawajia kama mtego. . .Mar 34.3

    Ulimwengu, ukiwa umejaa ghasia, ukiwa umejaa starehe zilizo kinyume na Mungu, utakuwa umelala, utakuwa umelala katika usalama wa kidunia. Watu wataona kuja kwa Bwana kuko mbali. Watayabeza maonyo. Watajigamba kwa kiburi, “Vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.” “Na kesho itakuwa kama leo. Siku kuu kupita kiasi.” 2 Pet. 3:4; Isa. 56:12. Tutazama zaidi katika kupenda starehe. Lakini Kristo anasema, “Tazama naja kama mwivi.” Ufu. 16:15. Wakati ambao ulimwengu ukiuliza kwa kejeli, “Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake?” ishara zitakuwa zikitimia. Wakati tukisema, “Amani na salama,” uharibifu utakuja kwa ghafla. Wakati mwenye kudhihaki, mwenye kuukataa ukweli, ameanza kupuuza; wakati kazi za kawaida katika kutafuta pesa zinafanyika bila kujali kanuni; wakati mwanafunzi akitafuta maarifa yote isipokuwa yale ya Biblia, Kristo atakuja kama mwivi.Mar 34.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents