Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mibaraka Kwa Wale Wanaokesha, Sura ya 28

    Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin nawaambieni, Atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia. Luka 12:37Mar 36.1

    Kila wakati Mungu amekuwa akitoa maonyo kwa ajili ya mapigo yanayokuja. Wale waliokuwa waaminifu kwa ujumbe uliotolewa katika wakati wao, na kuishi sawa na imani yao, wakitii Amri zake, waliepuka mapigo ambayo yaliwapiga waasi na wasioamini. Neno lilimjia Nuhu, “Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu.” Nuhu alitii na kuokolewa. Ujumbe ulimjia Lutu, “Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu” Mwa. 7:1; 19:14. Lutu alijiweka katika uongozi wa wale wajumbe kutoka mbinguni, na akaokolewa. Vivyo hivyo, wanafunzi wa Yesu walipewa onyo juu ya kuharibiwa kwa Yerusalemu. Wale waliokuwa wakiziangalia ishara za uharibifu uliokuwa unakuja, na kukimbia kutoka katika ule mji, waliepuka kuangamia. Vivyo hivyo sasa tunapewa maonyo juu ya ujio wa pili wa Kristo na uharibifu anaokuja juu ya ulimwengu. Wale wanaoyasikia na kuyashika maonyo wataokolewa.Mar 36.2

    Kwa kuwa hatujui bado saa halisi ya kuja kwake, tunaagizwa kukesha. “Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha.” Lk. 12:37. Wale wanaotazamia kuja kwa Bwana hawangoji bila kufanya kazi yo yote. Matarajio ya kuja kwa Kristo ni kwa ajili ya kuwafanya watu wamche Bwana, na kuziogopa hukumu zake juu ya makosa. Ni kwa ajili ya kuwaamsha waione dhambi kubwa ya kuikataa rehema yake aliyoitoa. Wale wanaomngoja Bwana wanatakasa nafsi zao kwa kuutii ukweli. Wanafanya kazi kwa bidii huku wakikesha kwa makini. Kwa kuwa wanajua kuwa Bwana yu mlangoni, bidii yao inahuishwa ili kushirikiana na viumbe wa mbinguni katika kazi ya kuokoa roho. Hawa ni watumishi wenye busara na waaminifu wanaowapa watu wa nyumbani mwa Bwana “posho kwa wakati wake.” Lk 12:42. Wanautangaza ukweli ambao ni kwa ajili ya wakati huu. Kama vile Henoko, Nuhu, Ibrahimu, na Musa walivyotangaza ukweli kwa ajili ya wakati wao, ndivyo watumishi wa Kristo wanavyotoa onyo sasa kwa ajili ya kizazi chao.Mar 36.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents