Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Chunguza Moyo Wako, Sura ya 41

    Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa. 2 Wakorintho 13:5.Mar 49.1

    Hakuna udanganyifu unaozidi ule wa dhambi. Ni mungu wa dunia hii ambaye analaghai, anapofusha, na kuongoza katika maangamivu. Shetani haingii na jeshi la majaribu kwa mara moja. Huyafunika majaribu haya na mwonekano wa wema. . . roho zilizodanganyika huchukua hatua moja, kisha huandaliwa kwa ajili ya hatua inayofuata ... Ah. . .Jaiti ungeona jinsi Shetani anavyotazama wakati chambo kikipokelewa kwa urahisi, na kisha kuona roho zikipelekwa katika njia aliyoiandaa. . .!Mar 49.2

    Upo umuhimu wa kufanya tathmini binafsi, na kufanya uchunguzi kulingana na neno la Mungu; je, niko sawa, ama nimeoza moyoni? Je, nimefanywa upya katika Kristo, au bado moyo wangu unatii tamaa za mwili, hali kwa nje nikionekana nimevikwa vazi jipya? Hebu jipeleke kimawazo kwenye mahakama ya Mungu, kisha jipime kwa nuru itokayo kwa Mungu na ugundue kama ipo dhambi yoyote, uovu wowote, au sanamu yoyote ambayo hujaitoa. Sali. . . kuliko wakati wowote uliopita, ili usidanganywe na hila za Shetani; ili usiswekwe katika ukaidi, kutojali na roho ya ubatili. . .Mar 49.3

    Mojawapo ya dhambi ambazo ni sehemu ya dalili ya siku za mwisho, ni Wakristo kupenda anasa kuliko kumpenda Mungu. Hebu shughulikeni kwa dhati kabisa na roho zenu wenyewe. Jichunguzeni kwa uangalifu. Ni wachache kiasi gani ambao baada ya kujichunguza kwa uaminifu, wanaoweza kuangalia juu Mbinguni na kusema “. . .Mimi sipendi anasa kuliko kumpenda Mungu.” Ni wachache kiasi gani wanaoweza kusema, “ya dunia yameshakufa ndani yangu. . .na wakati yule aliye uhai wangu atakapotokea, mimi pia nitatokea pamoja naye katika utukufu.”Mar 49.4

    Upendo na neema ya Mungu! Neema yenye thamani kubwa! Iliyo aghali kuliko dhahabu. Inainua na kuadilisha roho kuliko kanuni nyingine yoyote. Inaelekeza moyo na mapenzi yake Mbinguni. Wakati wale wanaotuzunguka wakifungwa na ubatili wa dunia, kutafuta anasa, na upuuzi, mazungumzo yetu yako mbinguni, mahali tunapompata Mwokozi; roho ikimkamata Mungu kwa ajili ya msamaha na amani, kwa ajili ya haki na utakatifu wa kweli. Mjadala na Mungu na tafakuri juu ya mambo ya mbinguni vinabadilisha roho na kuifanya iwe kama Kristo.Mar 49.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents