Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ng’oa Kila Mbegu ya Shaka, Sura ya 44

    Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ahadi. . .Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu. Waebrania 10:35-39.Mar 52.1

    Niliona kuwa tumo katika muda wa kutikiswa tayari. Shetani anajitahidi kwa nguvu zake zote kupokonya roho toka mkononi mwa Kristo na kuwasababisha watu hawa wamweke Mwana wa Mungu chini ya miguu yao. . .Mar 52.2

    Tabia inaendelezwa. Malaika wa Mungu wanapima viwango vya maadili. Mungu anajaribu na kuhakiki watu Wake. Malaika aliniambia maneno yafuatayo: “Jichungeni ndugu zangu, ili pasiwepo ndani ya mtu yeyote kati yenu moyo mwovu usioamini, upelekeao katika kumwacha Mungu aliye hai. Bali tianeni moyo ninyi kwa ninyi kila siku, maadamu ni leo; ili yeyote kati yenu asifanywe kuwa mgumu kutokana na udanganyifu wa dhambi. Tukizingatia chanzo cha ujasiri wetu bila kubadilika badilika hadi mwisho, tunafanywa kuwa washirika na Kristo.”Mar 52.3

    Mungu hapendezwi wakati yeyote kati ya watu Wake ambao wamekwisha jua uwezo wa neema Yake watamkapo wasiwasi wao, kwani kwa njia hiyo wanakuwa mfereji wa Shetani katika kusafirisha mapendekezo yao kwa akili za wengine. Mbegu ya kutokuamini na uovu ipandwayo haiwi rahisi kung’olewa. Shetani anairutubisha kila saa, na inachanua na kuwa na nguvu. Mbegu nzuri inapopandwa mahitaji pia kurutubishwa, kutiliwa maji, na kutunzwa kwa uangalifu: kwa sababu inatupiwa kila mvuto wenye sumu ili kuzuia ukuaji wake na kuisababishia kifo. Jitihada za Shetani zina nguvu sasa kuliko wakali wowote uliopita, kwani anajua ya kwamba muda wake wa kudanganya ni mfupi. . .Mar 52.4

    Watu wa Mungu watachekechwa, kama vile nafaka ichekechwavyo katika chekecheo, hadi makapi yatakapotengana na nafaka iliyo safi. Tunapaswa kumwangalia Kristo kama kielelezo na kuiga mfumo wake wa unyenyekevu. . . Nilioneshwa zawadi ya watakatifu, urithi usiokwisha. Kisha nikaoneshwa jinsi watu wa Mungu walivyovumilia kwa ajili ya ukweli, na liatima yake mbinguni pataonekana ni rahisi sana kupafikia. Walitathmini mateso yapatikanayo wakati huu na kuona hayakulingana kabisa na utukufu utakofunuliwa kwao. Watu wa Mungu katika siku hizi za mwisho watajaribiwa. Lakini mara baada ya jaribu la mwisho kuja, watapokea karama ya uzima wa milele.Mar 52.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents