Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Tumaini la Marejeo, Sura ya 4

    Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina, na uje, Bwana Yesu. Ufunuo 22:20Mar 12.1

    Kwa karne zote, kurudi kwa Bwana mara ya pili limekuwa ndilo tumaini la wafuasi wake wa kweli. Ahadi ya Mwokozi wakati akiagana na wanafunzi katika mlima wa Mizeituni, kwamba atakuja tena, iliangaza nuru katika siku za usoni kwa wanafunzi wake, na kuijaza mioyo yao furaha na matumaini ambayo yasingeweza kuzimwa na huzuni wala kuhafifishwa na majaribu. Katikati ya maumivu na mateso, “mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu” yalikuwa ni “tumaini lenye baraka.” Wakristo wa Thesalonike walipokuwa wakihuzunika wakati wa kuwazika wapendwa wao waliokuwa wameishi na kuamini kuwa wangeshuhudia kuja kwa Bwana, mtume Paulo, aliyekuwa mwalimu wao, aliwaelekeza kwenye ufufuo ambao utafanyika wakati Mwokozi atakaporejea. Ndipo wale waliokufa katika Kristo watafufuliwa, nao wataungana na watakatifu walio hai, na kwa pamoja watanyakuliwa ili wamlaki Bwana angani. Na hivyo akasema, “hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo.” 1 Thes. 4:16-18) Kutoka katika magereza yaliyo chini ya ardhi, nguzo za kuchomea watu moto, na majukwaa ya kunyongea watu, ambapo watakatifu na wafia dini walitoa ushuhuda wao juu ya kweli, daima huja maneno yanayoshuhudia imani na tumaini lao. Mkristo mmoja alisema, “Kwa sababu ya kupatiwa uhakika wa kufufuka kwake, na hatimaye ufufuo wao wenyewe wakati wa kuja kwake, hawakuogopa kifo, nao walipata ushindi.” Daniel T. Taylor, The Reign of Christ on Earth, The Voice of the Church in All Ages, uk. 33. Walikuwa tayari kufa, ili waweze “kufufuka wakiwa huru.” Walitazamia “Bwana aje katika mawingu ya mbinguni pamoja na utukufu wa Baba yake” “akileta majira ya ufalme kwa wenye haki.” Wa-Waldensia walishikilia imani hiyo. Wycliffe alitazamia marejeo ya Mwokozi kama tumaini la kanisa.Mar 12.2

    Akiwa katika kisiwa chenye miamba cha Patmo, yule mwanafunzi mpendwa alisikia ahadi hii, “Naam, naja upesi,” na jibu lake lenye shauku “Amina, na uje, Bwana Yesu,” linatoa mwangwi wa kile ambacho kimekuwa ni ombi la kanisa katika safari yake yote hapa duniani.Mar 12.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents