Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kristo: Mwokozi Pekee, Sura ya 65

    Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi. Wakolosai 1:13,14.Mar 73.1

    Bila kujali wewe ni nani au jinsi gani maisha yako yamekuwa, waweza tu kuokolewa kwa mpango pekee wa Mungu aliouweka. Ni lazima utubu; sharti uanguke kikamilifu katika Mwamba, Yesu Kristo.Mar 73.2

    Lazima uhisi hitaji lako la tabibu na hivyo hitaji lako la tiba pekee dhidi ya dhambi, ambayo ni damu ya Kristo. . . Damu ya Kristo itawafaa tu wale ambao wanajihisi kuhitaji nguvu yake ya utakaso.Mar 73.3

    Ni upendo na unyenyekevu wa kushangaza kiasi gani huu, kwamba tulipokuwa hatuna chochote kinachostahili rehema ya kimbingu, Kristo alikuwa tayari kufanyia kazi ukombozi wetu! Lakini masharti ya Tabibu wetu mkuu kwa kila roho ni kujikabidhi kwake bila maswali. Hatuhitaji kutoa suluhu kwa ajili ya kesi yetu wenyewe. Sharti Kristo awe ndiye mtawala wa juu wa nia zetu na matendo yetu. . .Mar 73.4

    Twaweza kujidanganya wenyewe. . . kwamba maadili yetu yamekuwa sahihi na kwamba hatuhitaji kujinyenyekeza wenyewe mbele za Mungu kama wenye dhambi tu. Lakini twapaswa kuridhika kuingia katika maisha kwa namna ile ile kama Mkuu wa wenye dhambi. Twapaswa kutupilia mbali haki yetu wenyewe na kuomba tupewe haki ya Kristo ambayo kwa asili hatustahiIi. Tunapaswa kuweka tegemeo letu kikamilifu kwa Kristo ili tuwe na nguvu. Nafsi sharti ile. I unapaswa kutambua ya kwamba vyote tulivyo navyo vinatokana na utajiri wa ajabu wa neema ya mbinguni. Hebu hii na iwe lugha ya mioyo yetu: “Isiwe sisi, Ee Bwana, siyo sisi, bali kwako wewe na uwe utukufu, kwa sababu ya rehema zako, na kwa sababu ya kweli yako.”Mar 73.5

    Baada ya imani ya kweli ni upendo, na upendo kwa njia ya utii. Uwezo wote na shauku za mtu aliyeongoka lililetwa chini ya utawala wa Kristo. Roho wake ni uwezo ufanyao yote kuwa mapya, akibadilisha wote wanaompokea wafanane na sura ya kimbingu...Mar 73.6

    “Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi.” Mtu huyu anahisi ya kwamba amenunuliwa kwa damu ya Kristo na amefungwa kwa viapo vitakatifu kwa ajili ya kumtukuza Mungu katika mwili wake na pia roho yake, ambavyo vyote ni vya Mungu. Kupenda dhambi na kujipenda nafsi vimeshindwa ndani yake. Kila siku mtu huyu huhoji: “Nimrudishie BWANA nini kwa ukarimu wake wote alionitendea?” “BWANA, nikufanyie nini?”Mar 73.7

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents