Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Onja,Sura ya 66

    Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini. Zaburi 34:8.Mar 74.1

    Je, sisi wenyewe twawezaje kujua wema na upendo wa Mungu? Mtunga zaburi anatuambia tusisikie tu na kujua, tusisome tu na kujua, tusiamini tu na kujua; lakini anasema “onjeni mwone ya kwamba Bwana yu mwema.” Badala ya kutegemea neno la mtu mwingine, onja wewe binafsi.Mar 74.2

    Uzoefu ni ufahamu upatikanao katika jaribio. Dini ambayo ina majaribio ndiyo inayohitajika sasa... Naam, baadhi wanao ujuzi kinadharia wa ukweli wa kidini, lakini kamwe hawajahisi katika mioyo yao uwezo wa kimbingu wa neema unaobadilisha. . . Wanaamini juu ya uwepo wa ghadhabu ya Mungu, lakini hawaweki jitihada yoyote kuikimbia. Wanaamini juu ya mbingu, lakini hawajinyimi chochote ili kuipata. . . Wanajua tiba ya dhambi, lakini hawaitumii. Wanajua kilicho sahihi, lakini hawakifurahii. Wanachokifanya tu ni kuongeza ufahamu wao unaoongeza hukumu yao. Kamwe hawajaonja na kujifunza kwa uzoefu ya kwamba Bwana ni mwema.Mar 74.3

    Kuwa mwanafunzi wa Kristo ni kukana nafsi na kumfuata Yesu ziwe nyakati za habari nzuri au mbaya. . . Kila mazoea yaliyoendekezwa yanayozuia uhai wa kidini sharti yaondolewe. . . Je, tutaweka jitihada katika kujinyima kulingana na thamani ya kitu tunachohitaji kukipata?Mar 74.4

    Kila aina ya mahusiano tunayoyatengeneza, hata yawe katika kiwango gani, hutuvuta. Kiwango cha kukubali kwetu mvuto husika kinatokana na kiwango cha kujihusisha kwetu na jambo lile linalotuvuta, mara ngapi tunajihusisha nalo, na upenzi wetu kwa ajili ya yule tunayehusiana naye. Kwa hiyo, kwa kumfahamu na kushirikiana na Kristo tutakuwa kama yeye, Yeye aliye kielelezo kisicho na kasoro.Mar 74.5

    Ushirika na Kristo. . . una thamani kubwa kiasi cha kushangaza! Ni upendeleo kwetu kuufurahia ushirika huo kama tukiutafuta, kama tutajinyima ili kuupata.Mar 74.6

    Kwa hiyo kila mmoja anaweza, kwa uzoefu wake binafsi, kuwa “ametia muhuri ya kwamba Mungu ni kweli.” Yohana. 3:33....Huyu atashuhudia: “Nilihitaji msaada, nikaupata kwa Yesu. Kila nilichotaka nilikipata, hitaji la roho yangu ilikidhiwa... Ninamuamini Yesu kwa sababu yeye ni Mwokozi wa kimbingu kwangu. Ninaiamini Biblia kwa sababu nimeitambua kuwa sauti ya Mungu kwa ajili ya roho yangu.”Mar 74.7

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents