Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Imani ya Wanamatengenezo, Sura ya 6

    Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. 1 Wakorintho 15:26.Mar 14.1

    Luther alitamka: “Kwa kweli ninashawishika ya kwamba haitapita miaka mia tatu yote kabla ya siku ya hukumu kuja. Haiwezekani kwa Mungu, na wala hatatenda hili: kuuacha ulimwengu muovu hivi kwa muda mrefu zaidi.” “Siku kuu inakaribia wakati ambapo ufalme wa machukizo utatupiliwa mbali.” -Daniel T. Taylor, The Reign of Christ on Earth; au The Voice ot the Church in All Ages, uk. 33.Mar 14.2

    “Dunia hii inayozeeka haiko mbali na mwisho wake,” alisema Melanchthon. Calvin anasihi Wakristo “wasisite, wakitamani kwa shauku siku ya ujio wa Kristo kama iliyo heri kuliko matukio mengine yote;” na anatamka kwamba “familia nzima ya waaminifu watadumu kuitazamia siku ile.” Anasema “Sharti tuwe na njaa ya kuwa na Kristo, tunapaswa kutafuta, kutafakari, hadi mapambazuko ya siku ile kuu, Bwana wetu atakapodhirisha kikamilifu utukufu wa Ufalme wake.”-Ibid., uk. 158, 134.Mar 14.3

    “Je, Bwana hakupaa na mwili kama wetu mbinguni?” alihoji Knox, Mwanamatengenezo wa Kiskoti, “na je, hatarejea? Twajua ya kwamba atarejea, tena kwa haraka.” Ridley na Latimer, ambao walitoa maisha yao kwa ajili ya kweli, walifanya hivyo wakitazamia kwa imani ujio wa Bwana. Ridley aliandika: “Hii ni imani yangu thabiti, ambayo pia ninaitamka - ya kwamba dunia inafikia mwisho wake. Hebu na tulie ndani ya mioyo yetu pamoja na Yohana, mtumishi wa Mungu, tumlilie Mwokozi wetu Kristo, Na Uje, Bwana Yesu, na uje.” -Ibid., kur. 151, 145.Mar 14.4

    “Mawazo ya ujio wa Bwana,” alisema Baxter, “ni matamu na ya kufurahisha kwangu.” Richard Baxter, Works, Vol. 17, uk. 155. “Ni kazi ya imani na ni tabia ya watakatifu wake kupenda ujio wake na kulitafuta tumaini hili lenye baraka.” “Kama mauti ni adui wa mwisho atakayeangamizwa katika ufufuo, twaweza kujifunza kwa makini jinsi waumini wapaswavyo kutegemea na kuomba kwa ajili ya kuja kwa Kristo mara ya pili, wakati huu ushindi wa mwisho ulio kamili utakapopatikana.” -Ibid., vol. 17, uk.500. “Hii ni siku ambayo waumini wote wanapaswa kuitamani, kuitegemea, na kuisubiri, kama kilele cha shauku zote, jitihada zote na kazi yote ya ukombozi.” “Fanya hima, Ee Bwana, kuileta siku hii ya baraka!” -Ibid., vol. 17, uk. 182, 183. Hilo ndilo lililokuwa tumaini la kanisa la mitume, tumaini la “kanisa jangwani,” na tumaini la Wanamatengenezo.Mar 14.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents