Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    “Uwe Tayari, Uwe Tayari, Uwe Tayari”, Sura ya 90

    ...Ujiweke tayari kuonana na Mungu wako, Ee Israeli. Amosi 4:12.Mar 98.1

    Kama Kristo angetokea leo mawinguni, ni nani angekuwa tayari kumlaki? Kama tungebadilisliwa na kuingizwa mbinguni katika hali ya tabia tulizo nazo leo. Je, tungekuwa tayari kuungana na watakatifu wa Mungu, kuishi katika mapatano mazuri na familia ya kifalme, au watoto wa Mfalme wa mbinguni? Je, umefanya maandalizi gani kwa ajili ya hukumu? Je, umefanya mapatano kati yako na Mungu? Je, unatenda kazi na Mungu? Je, unawatafuta ili uwasaidie wale walio karibu nawe, wale wa nyumbani mwako, wale walio jirani nawe, wale unaokutana nao ambao hawazishiki amri za Mungu?. . . Je, tunajitayarisha kukutana na Mfalme?. . .Mar 98.2

    Kama ingewezekana kuingizwa mbinguni jinsi tulivyo sasa, ni wangapi kati yetu tungeweza kutazamana na Mungu? Ni wangapi kati yetu tulio na vazi la harusi? Je, ni wangapi kati yetu tusio na doa au kunyanzi au kitu chochote kama hivyo? Je, ni wangapi kati yetu tu tayari kupokea taji ya uzima? Mtu hawi mtu kwa sababu ya cheo chake. Ni Kristo tu ambaye akikaa ndani ya mtu, mtu huyo anastahili kupokea taji ya uzima, ile isiyo haribika.Mar 98.3

    Nilielekezwa kuwaangalia masalio duniani. Malaika aliwaambia, “Je, utaweza kuepuka mapigo saba ya mwisho?. . . Kama ni hivyo, yapasa ufe ili uishi. Jiandae, jiandae, jiandae. Inawapasa kuwa na maandalizi makali kuliko mliyo nayo sasa. . . Toeni yote kwa Mungu. Wekeni yote madhabahuni pake- nafsi, mali na yote: kafara iliyo hai. Inahitajika kutoa vyote ili kuingia katika utukufu.”Mar 98.4

    Kristo anakuja kwa nguvu na utukufu mkuu. Anakuja na utukufu wake mwenyewe na ule wa Baba yake. . .Wakati waovu watakapokuwa wakikimbia mbali na uwepo wake, wafuasi wa Kristo watashangilia. . . Kristo amekuwa mwenzi wa kila siku na rafiki anayefahamika kwa wafuasi wake waaminifu. Wamekuwa wakiishi katika mahusiano ya karibu, katika ushirika wa kudumu na Mungu. Kwa hawa, utukufu wa Mungu umezuka.. . Sasa wanashangilia wakiwa kwenye miali mipevu ya mng’ao na utukufu wa Mfalme katika enzi yake. Wamejiandaa kwa ajili ya ushirika wa mbinguni; kwani wanayo mbingu mioyoni mwao.Mar 98.5

    Kama uko sawa na Mungu leo, basi uko tayari hata kama Kristo angetokea leo.Mar 98.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents