Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mahali pa Kuanzia Ushuhudiaji, Sura ya 94

    Wana wetu na wawe kama miche waliokua ujanani. Zaburi 144:12.Mar 102.1

    Kazi yetu kwa ajili ya Kristo inapaswa ianzie nyumbani katika familia. . . Hakuna eneo la kimishenari lililo muhimu kuliko hili.Mar 102.2

    Wamebarikiwa wazazi ambao maisha yao huakisi uungu kweli kweli, kiasi kwamba ahadi na amri za Mungu wanazozishika huwa zinaamsha tabia ya shukrani na kicho kwa watoto wao; hawa ni wazazi ambao huonesha wema, haki na uvumilivu, tabia ambazo huzaa kwa watoto upendo, haki na uvumilivu wa Mungu. Kwa kuwafundisha watoto kuwapenda, kuwaamini na kuwatii wazazi wao, wazazi hawa wanakuwa wamewafundisha watoto kumpenda, kumwamini na kumtii Baba wa mbinguni. Wazazi wanaowapa watoto wao karama ya namna hiyo, wanakuwa wamewawezesha kuwa na hazina iliyo ya thamani kuliko mali za karne zote - hazina inayodumu milele.Mar 102.3

    Mungu anataka kila mtoto wa umri mdogo kabisa awe mtoto wake, atwaliwe kuwa sehemu ya familia yake. Vijana waweza kuwa wadogo sana, lakini katika udogo wao wanaweza kuwa washirika katika jumuiya ya imani na kupata uzoefu mzuri sana. Wanaweza kuwa na mioyo iliyo laini na hivyo wakawa tayari kupokea fikra zitakazokuwa za kudumu. Wanaweza kuruhusu mioyo yao ivutwe na ujasiri na upendo wa Yesu, na kuishi kama Mwokozi. Kristo atawafanya kuwa wamishenari wadogo. Mkondo wote wa mawazo yao utabadilishwa, ili kwamba dhambi isionekane kuwa kitu cha kufurahisha, bali kitu cha kukataliwa na kuchukiwa.Mar 102.4

    Wazazi wanapaswa kufundisha watoto wao kwa kanuni na vielelezo kuhangaikia wale ambao hawajaujua ukweli. Watoto wanapaswa kuelimishwa kuhurumia wazee na walioteswa na watafute namna ya kuwapa nafuu maskini na walio katika dhiki ..Hebu wafundishwe tokea mapema katika maisha yao tabia ya kujinyima na kujikana nafsi kwa ajili ya wengine na kwa ajili ya kuendeleza kazi ya Kristo, ili wawe watendakazi pamoja na Mungu Mar 102.5

    Ni kusudi la Mungu kwamba familiazilizopo hapa duniani ziwe kielelezo cha familia ya mbinguni. Nyumba za Kikristo ambazo zimejengwa na kuendeshwa kulingana na mpango wa Mungu, ni moja kati ya mawakala wenye nguvu sana katika zoezi zima la ujenzi wa tabia ya Kikristo na maendeleo ya kazi yake.Mar 102.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents