Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Maranatha - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuhubiri Kwa Nguvu, Sura ya 108

    Siku zile aliondoka Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema “Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” Mathayo 3:1,2.Mar 116.1

    Katika maisha yake jangwani, Yohana Mbatizaji alifundishwa na Mungu. Alijifunza ufunuo wa Mungu katika viumbe vya asili. Alijifunza magombo ya manabii chini ya uongozi wa Roho wa Mungu. Kristo alikuwa fundisho lake, tafakuri yake, mchana na usiku hadi mawazo, moyo na roho vilipojazwa na njozi yenye utukufu.Mar 116.2

    Alimtazama Mfalme katika uzuri wake, kiasi cha kusahau nafsi yake mwenyewe. Aliona ukuu wa utakatifu wake na akajijua kama mtu asiyefaa na asiyestahili. Alikuwa atangaze ujumbe wa Mungu. Alikuwa asimame kwa nguvu ya Mungu na haki yake. Yohana alikuwa tayari kwenda kama mjumbe wa Mbinguni hata bila kuwa katika hali ya kuvutia kwa watu, kwa sababu aliutazama Uungu. Alisimama bila hofu mbele za wafalme wa kidunia kwa sababu alikuwa ameshanyenyekea kwa kutetemeka mbele za Mfalme wa wafalme.Mar 116.3

    Yohana alitangaza ujumbe wake bila ya maelezo marefu na maneno yaliyopangwa kwa urembo. Sauti yake iliyostua na iliyokuwa imara, hali ikijaza tumaini, ilisikika tokea jangwani: “Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” Mt. 3:2. Kwa jinsi ilivyokuwa mpya na yenye nguvu sauti hii iliwaamsha watu. Taifa zima IiIitikiswa. Umati wa watu ulimiminika kwenda jangwani...Mar 116.4

    Katika kizazi hiki, kabla tu ya kuja kwa Kristo mara ya pili katika mawingu, kazi kama ile ya Yohana inapaswa kufanyika. Mungu anaita watu ambao wataandaa wengine tayari kusimama katika siku ile kuu ya Bwana... Kama watu waaminio katika ujio wa Kristo ulio karibu, tunao ujumbe wa kutangaza — “Ujiweke tayari kuonana na Mungu wako.” Amo. 4:12. Ujumbe wetu unapaswa usipinde kama ule wa Yohana ulivyotolewa bila kupinda. Aliwakemea wafalme kwa sababu ya uovu wao, bila kujali ya kuwa maisha yake yalikuwa hatarini, hakusita kutangaza neno la Mungu. Vivyo hivyo kazi yetu katika kizazi hiki yapaswa ifanyike kwa uaminifu.Mar 116.5

    Ili tutoe ujumbe kama Yohana alivyoutoa, tunapaswa kuwa na uzoefu wa kiroho kama yeye. Kazi hiyo hiyo inapaswa kufanyika ndani yetu. Tunapaswa kumtazama Mungu, na katika kumtazama Yeye tuweze kusahau nafsi zetu.Mar 116.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents