Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu”, Sura ya 109

  Tazama Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! Yohana 1:29.Mar 117.1

  Kwa asili, Yohana alikuwa na mapungufu na udhaifu ulio kawaida ya wanadamu: lakini mguso wa upendo wa Mungu ulimbadilisha. Baada ya huduma ya Kristo kuanza, wanafunzi wa Yohana walikuja kwa Yohana wakilalamika ya kwamba watu wote walikuwa wakimfuata Mwalimu mpya, Yohana akaonesha kwao kwa uwazi kabisa jinsi alivyoelewa uhusiano kati yake na Masihi, na pia jinsi alivyofurahi kumkaribisha Yeye ambaye alikuwa amemtayarishia njia.Mar 117.2

  “Hawezi mtu kupokea neno lolote,” alisema, “isipokuwa amepewa kutoka mbinguni. Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. . . Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.” Yn. 3:27-30.Mar 117.3

  Hali akimwangalia Mkombozi kwa imani, Yohana aliinuka hadi kiwango cha kukana nafsi. Hakuvutia watu kwake, bali aliwainua mawazo yao juu zaidi, hadi katika pumziko la Mwana-kondoo wa Mungu. Yeye mwenyewe alikuwa sauti tu, kilio katika jangwa. Sasa alikubali kwa furaha ukimya na kutoonekana, ili macho ya wote yageuziwe kwa Nuru ya uzima.Mar 117.4

  Wale walio wa kweli katika wito wao kama wajumbe wa Mungu hawatafuti heshima kwa ajili yao binafsi. Upendo kwa Kristo utameza kujipenda nafsi. Hawa watatambua ya kwamba ni kazi yao kutangaza, kama alivyofanya Yohana Mbatizaji: “Tazama Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Yn 1:29. Watamwinua Yesu, na pamoja naye ubinadamu utainuliwa. . .Mar 117.5

  Roho ya nabii, hali ikiwa imeondolewa ubinafsi, ilijazwa na nuru ya Uungu.. Alishuhudia utukufu wa Mwokozi. . . Wafuasi wake wote wanapaswa kushiriki utukufu huu wa Kristo.. .Twaweza tu kupokea amani ya mbinguni kama tupo tayari kukana nafsi. Twaweza kuiona tabia ya Mungu, na kumkubali Kristo kwa imani, ikiwa tu tutakubali kukabidhi kila wazo katika kumtii Kristo. Wote watendao hili watapewa Roho Mtakatifu bila kipimo. Katika Kristo “unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. Na ninyi mmekamilika katika Yeye.” Kol. 2:9,10.Mar 117.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents